Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Mnakumbuka zile kamata kamata za wapinzani na wafanyabiashara? It seems kama ACT Wazalendo wamekuja na muarubaini wa tatizo hilo
Kiongozi mstaafu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema endapo chama hicho kitapewa mamlaka na wananchi katika uchaguzi wa Serikali za mitaa, kitahakikisha kinadhibiti ukamataji holela unaotajwa kufanywa na Jeshi la Polisi bila ya kutoa taarifa kwenye serikali ya kijiji au kitongoji.
Soma pia: itto Kabwe: Sitagombea Urais 2025, nitarejea kuimarisha Bunge
Akizungumza wakati akifungua kampeni za ACT za uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika kijiji cha Songambele kilichopo kata ya Uyowa, jimbo la Ulyankulu mkoani Tabora, Novemba 20, 2024, Zitto Kabwe amesema ni muda mwafaka wa kuhakikisha utaratibu wa ukamataji watu unafuatwa, na kwamba hilo litawezekana tu ikiwa tu kutakuwa na utawala mzuri wa sharia ngazi ya kijiji utakaowekwa na chama hicho endapo kitapewa ridhaa
Sambamba na hilo. kiongozi huyo amesema chama chake kikipata ridhaa kitakomesha rushwa katika ofisi za vijiji kwa kuhakikisha kinatoa huduma bure kwa wananchi.