ACT - Wazalendo kabla ya kukubali kuingia kwenye "SUK" walikaa vikao kadhaa na Balozi Wa Marekani.
Leo Balozi Wa Marekani amekua wa kwanza kupongeza hatua ya ACT - Wazalendo kukubali SUK.
Tundu Lissu na ACT - Wazalendo ndio wataisababishia madhara makubwa sana serikali ya CCM muda si mrefu (Japokua mpaka sasa hivi wameshaijeruhi sana tu, ila wanaficha ukweli na kujikaza kiaskari). Wengi watalidharau hili na kulipinga.
Mwaka huu na mwakani serikali "ITAKOPA SANA NA KUJILIMBIKIZIA MADENI MENGI SANA", ambayo mpaka wajukuu zetu watayakuta.
Sisi watanzania wengi tunakwenda kwa kufuata mkumbo. Hio picha ni foundation ya sinema inayojiri muda si mrefu ya kesi ya ICC na African Court On Human And Peoples Rights.
Stay tuned. Yajayo yanafurahisha.
Mkuu mwenye jina kubwa la wavumbuzi wa kikoloni,
1. Tundu Lissu and ACT-WaZALENDO kabla ya madhara unayobashiri kuisababishia serikali ya Tanzania usahau nahau hiyo haipo, na haitakuwepo maana wanachokifanya wakiwa wamelala, wanatembea, wakiongea, wakiwaza mahali popote walipo kabla ya utekelezaji wake watajuta kwanini walihadaika kuingia kwenye njama hizo;
2. Hiyo mahakama yako ya ICC unayoihubiri kila kukicha utaendelea kuisikia hadithi zake mpaka Mungu anakutwaa bila kushuhudia kwa macho na masikio yako kile unachotamani kitokee dhidi ya Tanzania
3. Wewe na genge lako inaonesha una chuki binafsi dhidi ya CCM, serikali na viongozi waandamizi wake kwa sababu zako mwenyewe na wengine wenye mawazo OVu kama ya kwako;
4. Hakuna haki wala utu bila wajibu kwa matendo na maneno yako na kufanya kazi halali kwa bidii kujiletea maendeleo mwenyewe kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya mifumo ya kukuza uchumi na kuimarisha usalama wa kila mtu na taifa kwa ujumla;
5. Taifa namba moja linaloongoza kwa uvunjifu wa haki za binadamu ni Marekani (mauaji na mifarakano/migogoro ya kivitayanayotokea nchi za Uarabuni, Afrika nk ni kwa hiasani yake), jumuiya ya nchi za Ulaya kulazimisha desturi na tamaduni zao zitekelezwe na nchi za Afrika ni zao la UOVU mkuu;
6. Kama uko Tanzania au umejificha mahala pengine nje ya nchi halafu unachochea chuki hizi sasa kesho itakumaliza mwenyewe na hutakuwa na kauli ya kuungama matendo yako hayo;
7. Siasa ni tiba ya hisia za kufikirika lakini haileti uzima kwa watu; kumbuka mwili umeundwa kati sehemu tatu kuu zenye kukamilisha utambulisha wa binadamu : a) Mwili b) Nafsi na c) Roho na ili binadamu akamilike ni wajibu azaliwe, aishi kwa kiwango chchote cha muda wa uhai, afe na aoze kisha matendo yake yahesabiwe faida yaliyoleta.
Wewe matendo yako yanadhihirisha hayana ROHO ila yameegema sana kwenye matamanio ya Nafsi na Mwili ambavyo matendo yake baada ya kufa hayatoi hesabu ya tija.
Tafadhali heshimu Tanzania, WaTanzania na Viongozi wake.