Uchaguzi 2020 Zitto Kabwe: Viongozi wa Upinzani tulikaa pamoja tukakubaliana kwa Upande wa Urais asimame Tundu Lissu

Uchaguzi 2020 Zitto Kabwe: Viongozi wa Upinzani tulikaa pamoja tukakubaliana kwa Upande wa Urais asimame Tundu Lissu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Kiongozi wa cha chama cha ACT-Wazalendo taifa Zitto Kabwe amesema endapo wananchi wa mkoa wa Katavi watawachagua viongozi wa upinzani watahakikisha wanaletea mabadiliko katiko sekta ya afya, maji na elimu.

Ameyasema hayo alipokua akizungumza na wananchi wa manispaa ya Mpanda katika uwanja wa Sikonge na kusema kuwa a endapo watapata ridhaa upinzani watahakikisha wanatatua kero za wakulima sambamba na kuboresha maisha ya watanzania.

Aidha, amewaomba wananchi wa jimbo la Mpanda mjini kumchagua mgombea ubunge kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Rhoda Kunchela na kusema kuwa wao kama vyama upinzani wameona ni vyema kusimamisha wagombea wanaoweza kumshinda mgombea wa CCM.

Akizungumzia nafasi ya urais kiongozi huyo amesema viongozi wa upinzani wamekaa kwa pamoja na kuona ni vyema kumsimamisha mgombea urais kupitia chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Tundu Lissu.

Chanzo: Mpanda Radio
 
Pole Zitto Kwa ajali!! Mungu akupe nafuu ya haraka ili urudi katika majukumu yako, bado ni Kijana na unahitajika Sana katika Taifa lako Tanzania

Lakini tusikufiche, Muungano wenu huo... haumfanyi chochote JPM... Yeye ndiye anayesubiri kuapishwa!!

Muungane ama msiungane,ushindi wake upo pale pale!! Ukweli mchungu
 
Kitu Magufuli anasahau au anafanya kusudi ni kwamba;Watanzania hawataki kubaguana kwa kutumia
Kabila
Dini
Ukanda
Uvyama
Sasa ninachokiona kwa kiongozi huyu anajitahidi kutugawa kwa kutumia vyama. Naona upinzani unatumia nafasi hiyo kutuunganisha,
Ninavyo ona mimi kwa Tanzania kutugombanisha kwakutumia vyama imegonga mwamba, labda polisi wabariki hili lakini najiuliza na nimekosa majibu nikuulize mgombea wa Polepole iwapo utabahatika kuwapata washindi wote watokane na chama chako lengolako nini?hapo baadae!
 
Pamoja na kuungana lakini bado hakuna impact yeyote.
Ninachoona ni wapinzani wameongeza kiwango cha malalamiko kuliko mapambano ya sera nzuri na zenye mvuto.
 
Ni muda muafaka sasa kwa Membe kujitoa rasmi.
Practically Membe alishajitoa kitambo sema watu walishindwa kuielewa ile tweet yake aliposema "Mimi ndie mgombea wa ACT"

Wakati ule wakati raia tunazungumzia suala la Membe kujitoa kulikuwa yanafanyika mazungumzo kati ya ACT na CHADEMA... this's politics, sio kwamba mtu anajitoa tu from nowhere bila kujua atapata nini na atapoteza nini! Usiseme mbona CHADEMA kule Zanzibar walimuunga mkono Seif bila hiyo milolongo cuz' I believe both, you and I tunafahamu kwanini!!

So, hivyo ndivyo walikuwa wanajadiliana lakini kabla hawajafikia tamati, watu wakatoa fake info kwamba Membe anaiunga mkono CHADEMA wakati ilikuwa bado haijawa official...
 
Yes Zitto, umesomeka!! Haya ndiyo maneno watanzania wanataka kuyasikia kwa sasa!!
Sawa kabisa. Lakini wamechelewa sana. Kwenye uraisi kuna kura zitapotea sana kwenda kwa Membe sababu jina litakuwepo.
Wamechelewa sana hawa kuungana.
 
Nadhani alishasema kwamba anamuunga mkono Lissu kugombea Urais?
Kusema haitoshi, AJITOE ili jina lake LISIWEPO kwenye BALLOT PAPER.
Ccm watazigawa kura za Lisu na kumpa Membe ili ,ionekane kashindwa kihalali.

Jamani mnadhani kwanini CCM na NEC wanalazimisha wagombea waendelee kuwepo?!

NRA hawapigi kampeni, NCCR hivyo hivyo, DP wanamgombea urais afanyi kampeni, kwanini sasa wanashiriki?!

Mbinu hizi mzielewe, MEMBE ajitoe official na aondolewe kwenye karatasi za kupiga kura, huko ndio kumiunga mkono LISU sio vinginevyo.
 
Yes Zitto, umesomeka!! Haya ndiyo maneno watanzania wanataka kuyasikia kwa sasa!!
Ameshachelewa angewahi mapema.
Sasa hata wakiungana hawatazidi.kuwa milioni 3
Sasa hapo watashinda wapi?
Labda washinde njaa.
 
Back
Top Bottom