Zitto: Makubaliano ya Serikali na Barrick Gold changa la macho

Mpinzani wa kupinga. Yeye (Zito) awamu ya nne ndiye alikuwa mstari wa mbele kusema kuwa kinana ni mwizi mkuu wa rasilimali za taifa. Kuwa ni jangiri maarufu wa meno ya tembo. Ajabu hivi sasa yeye ndiye mtetezi mkubwa wa Kinana. Hivi huyu binadamu ni binadamu wa aina gani?
 
Mimi na wenzangu wa timu yetu tunakanusha hii taarifa ya Zitto na sio Mzalendo..tutasema yakutungwa na nimaelekezo ya Mabeberu. Kwa sisi kila maamuzi ya Rais na Mwenyekiti wetu ni sahihi tuu..😄😄. Msinipopoe jamanii..🏃🏃
 
Zitto kama chama umempa Maalim Seif bure huwezi kuelewa haya mambo.
 
Kulinda aibu yao ndio wametuingiza chaka zaidi,kama yalioandikwa hapa yana ukweli hata kwa 25% tu basi tumeumia viaya mno!!!!
Nilikuwa najiuliza,kwanini hawa barrick wanapigana sana vita na Acasia juu ya hisa za Acasia,kumbe washaona chaka la kutupiga hela!!!!
Nchi imelaaniwa hii!
 


Tunamlaaani Zitto na timu ya Mabeberu walioamua kuweka document ya SIRI hadharani.. Mabeberu sio wa kuwachekea kabisa ni wachochezi sana..

😂😂😃
 
Mkuu njoo na hoja ya kumjibu kutokana na mada yake hapo juu ueleze jibu ya kila point yake hapo na ufafanuzi na faida tutakayo ipata kuendelea kumpa majibu kama haya ulio yaleta ni kuendelea kumpa kichwa ndugu huyu tusikwame kiasi hiki kwa kuja na vioja mimi ni mwana CCM ila ningefurahi kwa mwana chama mwenzangu mwenye uelewa na hivi vitu waje kumjibu vizuri kupangua hoja moja mpaka nyingine ili kumfedhehesha huyu kiumbe mnafiki zitto
 
Sasa mshauri wa uchumi wa Magu ni Maaga Mulagi a.k.a Syprian Musiba kaka Zitto , hatuwezi kutarajia jambo jema kutoka hizi akili za matope...uchafu kichwani uchafu katika maamuzi na utendaji!
 
Kama ni kweli basi nchi hii imelaaniwa!
 

Mkuu kama hii nchi watu wengi tungekuwa tunafikiri na kupambana kwa hoja kama hizi za ZZK tungefika mbali sana, hili suala ni critical sana na linahitaji majadiliano ya kina sana kama Taifa kuanzia bungeni, chamani na vikao nyeti vya serikali..

Leo hii akina Lusinde, Msukuma nk wako busy na press za siasa na hutasikia wakijadili vitu kama hivi..
 
Mi nadhani kufananisha makosa ya Chief Mangungo na makosa tunayoyafanya kizazi hiki ni kumkosea adabu chief huyo.

Kwa kipindi kile angeweza kupata wapi kujua thamani ya kioo, shanga na vitu vingine....! Lakini sisi kila kitu kwa sasa kinajulikana lakini tunachokifanya hakika hata mangungo angejinyonga kwa kujilaumu kwa alichokifanya.

Ni bahati mbaya kabisa Tanzania haijawahi kupata kiongozi mzalendo wa kweli kwa sababu jamii kwa ukubwa wake imekuwa "corrupt" hivyo ni wachache mno wenye kujali maslahi ya Taifa. Wengi hata tunaoibua madhaifu na ufisadi ni kwa ajili ya kujijenga kisiasa tu akishashika nafasi tunabaki kushangaa alivyobadilika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…