Zitto, Mbowe na Maalim Seif, hamuwezi kufungua kesi kwa hati ya dharura kudai kukamilishwa kwa mchakato wa Katiba Mpya?

Zitto, Mbowe na Maalim Seif, hamuwezi kufungua kesi kwa hati ya dharura kudai kukamilishwa kwa mchakato wa Katiba Mpya?

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Hili jambo nimeliongea humu mara nyingi ila leo nimeona nilirudie ile kwa style tofauti kidogo ya kutaja viongozi wa vyama vya siasa wakiwa ndio viongozi wakuu wa vyama vya upinzani.

Hapa Mbatia sijamtaja kwasababu naoni ni kama yuko vacation (hasikiki kabisa na sijui kapatwa na nini).

Tukirudi kwenye hoja ya msingi, wapinzani tambueni muda unayoyoma huku karibu wote mkiwa na kesi na hatujui hizi kesi zitaishaje (kumbukeni ya Sugu) hivyo ni bora wakati huu mkiwa bado mko huru ongezeni vyama vyenu katika kufungua kesi kwa hati ya dharura (kama kisheria inawezena ) kuiomba mahakama iiamuru serikali kukamilisha mchakato wa kura ya maoni ambao ndio kwa sasa umebaki.

Katiba mpya japo ina mapungufu na tuliipinga, lakini itaweza kutupatia Tume Huru yenye unafuu na kikubwa ita-facilitate kurekebishwa kwa sheria ya uchaguzi ili tuondokane na wakurugenzi wa Halmashauri kuwa wasimamizi wa uchaguzi.

Tukipata wabunge wengi wa upinzani itakuwa ni hatua nzuri na ni pia itakuwa ni mafanikio makubwa kwa upinzani kuelekea kushika dola siku za usoni.

Hivi mmejiuliza mkifungwa wote au baadhi yenu(hatuombei ) kama alivyofungwa Sugu hamuoni itawathiri sana katika haya mapambano maana mtakuwa mmeshasambaratishwa?

Na je mkitoka ndio muanze mchakato huo muda utakuwa unawasubiri?

Na hata kama kisheria inawezeka zile kesi za kudai Tume Huru na ile ya kupinga uchaguzi nazo muwashauri waliozifungwa wazifungue upya kwa hati ya dharura kwa hoja kuwa kuna chaguzi ndogo zinakuja wakati wowote kutokana na kujiuzulu kwa baadhi ya madiwani wa vyama vya upinzani.

Wapinzani komaeni wakati ni huu na mkumbuke wapinzani karibu wote mna kesi hivyo changeni mapema karata zenu.

Yote mnayoyapigia kelele sasa kama hiyo trilioni 1.5, watu kutekwa na kuwawa na mengineyo mengi bila katiba mpya au Tume Huru ya Uchagui kwa hakika haya yote ni bure na hakuna kitakachofanyika sana sana mtaishi kujiongezea umaarufu tu wa kisiasa ila lengo la nyie kushika dola litabaki kuwa ni ndoto.

Tutazame mbele vinginevyo miaka yote tutakuwa ni watu wa kulalamika tu na itakuwa haina maana kama tutaendelea kulalamika bila kufanya kile kilicho ndani ya uwezo wetu kwanza then tukishindwa ndio tuwe na uhalali wa kulalamika au kufikiria kuchukua maamuzi magumu.

Kwa sasa mnaweza msinielewa ila machungu ya kufanyiwa figisufigisu yakianza mtakumbuka ushauri huu.

The earlier the better.
 
Eeh Mwenyezi Mungu tuponyeshee Lissu wetu na umpatie ujasiri na nguvu ya kuwashinda maadui wake kwa maslahi mapana ya Taifa letu..!!!
 
Kwa ujumla sielewi faida ya wabunge wa upinzani kupoteza muda wao kuwa bungeni maana hawabadilishi chochote.

Ilikuwa muhimu zaidi kwa wapinzani kukusanya nguvu zao zote pamoja na za Watanzania wenye dhamira njema, kuhakikisha tunapata katiba mpya inayopunguza madaraka ya Rais na kupata Tume huru ya Katiba.

Wapinzani wameyafanya mambo yenye umuhimu mdogo kuwa makubwa na makubwa wameyafanya kuwa madogo.

Ubunge wanaoufurahia kwa sasa, bila katiba mpya, kwa kiwango kikubwa wanaufurahia kwa mara ya mwisho.
 
Back
Top Bottom