Inasikitisha sana kuona watu mahiri ndani ya JF wanashindwa kuunganisha dots.
Zitto kabwe alikubaliana kununuliwa mitambo ya kitapeli iliyotumika ya Dowans. Mwakyembe walikataa kwani kukubali kununua mitambo ya kitapeli, michakavu ni kukumbatia uozo na kuenzi rushwa na kukubali wezi kutuamulia mambo.
Kamati ile ilitoa mapendekezo ikiwa ni pamoja na tanesco kununua mitambo mipya kwa kipindi muafaka, na walisema kama tulikuwa tunatumia dola milioni 67 kununua mitambo iliyotumika ya dowans basi tunaweza kununua mitambo mipya kwa kiasi kama hicho na kutoa zaidi ya megawatt 100. Tanesco ilikuwa na muda wa kutosha wa kufanya hivyo na hawakufanya.
Dr idrisa aliahidi nchi kwenda gizani isiponunuliwa mitambo ya dowans kama vile viwanda vya kutengeneza jenereta vimefungwa, na kama fedha ilikuwepo ya kununulia mitambo ya dowans kwanini wasingelitumia fedha hizo kununulia mingine????
Zitto hakuwa sahihi na hawezi kuwa sahihi kuungana na akina Rostam kuwasaidia kufanikisha mbinu zao mbovu na uhujumu uchumi, Dr idrisa akiwa kama mdhamini wa mkopo wa mitambo ya richmonduli lazima afanye linalowezekana mitambo iende tanesco, sina uhakika Zitto anafaidika na nini?
Nchi kwenda gizani kamati ya akina mwakyembe ilifanya kazi yao kwa ufanisi mkubwa, na tanesco wakisaidiana na wizara ya nishati na madini ndio wazembe na wahujumu uchumi, wanatakiwa wajiuzulu kwa kushindwa kuwa na uwezo wa kutatua tatizo la umeme.
Watanzania wenzangu muda umefika wa kuanza kutafakari na kutumia maono kuelewa nini kinachotengenezwa, ni uhayawani kuamini kutotumia mitambo ya dowans ndio chanzo cha nchi kuingia gizani. Huu ni wizi na ukosefu wa kufikiri.
Nina watakia kila la kheri watanzania na kumwomba mungu watanzania waweze kuelewa ni jinsi gani wanavyochezewa akili zao na wezi na watawala wanaotumia jasho lao, wakiwaacha gizani wakati kwenye nyumba zao kuna jenereta, solar, nk na kuwatisha bila ya dowans hakuna tanzania yenye mwanga.Wizi na uhujumu umekuwa ni mtindo wa biashara Tanzania.