Zitto na chama chake wametufumbua macho,serikali ya CCM iliua na kuteka watu. Baadhi ya waliohusika wapo hai wafikishwe kortini

Zitto na chama chake wametufumbua macho,serikali ya CCM iliua na kuteka watu. Baadhi ya waliohusika wapo hai wafikishwe kortini

ACT ni mbia wa SMZ na Zitto ni Kiongozi Mkuu wa hicho chama.

Wangeonesha mfano kwa kuwafikisha kortini wauaji wa Uchaguzi Mkuu 2020 huko Zanzibar.

Well, ushaur mzur sana ila hata hili waloanza nalo ni muhimu pia then wataendelea na hayo ya znz!! Lkn msipige vita hii hoja aliyonayo coz ni muhimu kwa ustaw wa Taifa na uwajibikaji.
 
Naona huko twita anapost bila hata kuficha kitu. Anadai kuwa Akina Ben, Azory na wengine wengi ni wahanga.

Kwa hiyo kama ndio hivi wahusika watakuwepo mitaani huu ndio wakati wa kuwapeleka kortin.
Pamoja na kuwa utawala wa mwendazake kuwa na mabaya yake, lakini ni vyema kwa kiongozi ampingaye akiwa kama fanani kuchagua maneno ya kuongea pale wanapokuwa wakiwasiliana na hadhira. Ni vyema kutambua mambo yaliyofanywa na JPM bado yapo vichwani mwa watu wengi.

Lipo kundi kubwa la watu wengi wa hali ya chini ambao walimuunga mkono kwa sababu za kiushabiki, hasa kutokana na fursa alizowapa katika kuendesha maisha yao kwa njia zisizokuwa rasmi. Kundi hili halitambui sura ya halisi ya mkono wa chuma na madhila hasi yaliyofanyika kwa amri ya kipenzi chao.

Kuongea sana bila ya kutambua hisia na uelewa wa wale unaowaambia, kunaweza kuleta tafsiri tofauti. Jambo la msingi sana ni kujenga hoja zenye vielelezo na takwimu zisizokuwa kuwa na shaka yoyote ile.
tapatalk_jpeg_1557319509156.jpg
 
Back
Top Bottom