Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 239
Advocate Jasha, mkuu salamu zako! Zitto hajamalizwa kisasa bali kajimaliza kisiasa. Hakuna mtu aliyemtuma ashikilie bango ishu hili la Dowans. Kama alikuwa ana lolote la kusema angesema tu lakini si kulitetea hivyo na kujibu electronically kama vile yeye anajua vyote.Hapa kunamchezo mchafu ambapo mafisadi wanataka kuua ndege wawili kwa jiwe moja.1.Kumaliza Zitto kisiasa 2.Kutumia umaarufu wake kuwashawishi watu kununua mitambo hiyo nimemsikiliza Zitto katika mahojiono yake hapa MAGAZETI YA TANZANIA VIA KENNEDY amezungumzia umuhimu wa kuzikutanisha kamati zote zinazohusika pamoja na Tanesco wizara na serikali kujadili tatizo hili ili kuondoa vaccum iliyopo kwani hapa kuna mazingaombwe.Kama Tanesco inakimbia kutoka katika kamati hadi kamati badala ya kukutanisha pande zinazohusika.Hawa mafisadi walipanga na kizicheza karata zao kwa makini na kusubiri muda mbadala wa kuishinikiza serikali kununua mitambo hiyo kwa vitisho vya kua taifa litabidi kubaki katika giza.Kwa makusudi kabisa hawakuchua hatua zozote za kuziba mapengo yaliyowachwa na baada ya kuvunja mikataba na mikataba mingine kumalizika?kama kuna.watts 140 zimepungu baada ya kuvunja mkataba walisubiri nini kutafuta njia nyingine za kufua umeme?Niwazi kwa makusudi walivuta muda ambao umeme utakua unahitajika na muda wa kununua mitambo utakua finyu au haiwezekani na kuacha alternative ya kununua mitambo hiyo.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Unajua uchaguzi mkuu wa Tanzania umekaribia, sasa kuna namna inayofanywa ili kummaliza Zitto Zuberi Kabkwe (ZZK) kisiasa.
Hata akiitwa DOWANS yeye kama yeye hapungukiwi na kitu chochote kile.
Hao nao wamekosa kazi!kwani wakimwita Do'ns wanampunguzia nini?any way wanajifurahisha kwenye kahawa na muda unapita
Binafsi sioni kama kwa hili Zitto eti amejimaliza. Nadhani wengi hawakuelewa na hata hawataki kuelewa point ya Zitto. Halafu timing issue, wakati anatoa mapendekezo yake yale kuna baadhi ya vitu ambavyo havikuwa bayana. So I still find him as a VERY STRONG PERSONALITY ambayo ina THINK BIG. So sioni haja ya kumkatisha tamaa kwa issue hii ambayo iko wazi na logical.
Hawa jamaa wa KIGOMA wana matatizo ukishawapa pesa kidogo tu wAnasahau. INANIKUMNBUSHA YULE DR. WALID KABOURU hivi aliishia wapi? Wahenga walisema ukiwa mwongo usiwe msahaulivu. Jina alilopewa linamfaa kwani huyo DOWANS hatujamwona yeye anasema tununue mtambo kwa manufaa ya taifa basi yeye ndiye Dowans. Kama anabisha atuambie basi nani mmiliki wa DOWANS.
Hivi wakuu hapa JF kuna kidude mtu akitoa post nzuri unayokubaliana nayo unabonyeza "Thanks" Je kama mtu ametoa kitu kika Kubore unabonyeza wapi?
---Sipendi sana Generalisation of People. Eti jamaa wa KIGOMA!