OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Kiongozi Mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema gari namba T 249 CMV inayotajwa na Jeshi la Polisi kuwa imetumika na Watekaji kumteka Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana Taifa wa ACT, Abdul Nondo, inamilikiwa na Mtu anayeitwa Deogratius Beda Minja.
Pia soma: Kuelekea 2025 - Dar: Abdul Nondo amechukuliwa na Watu wasiojulikana katika mazingira ya utatanishi Kituo cha Mabasi cha Magufuli
Zitto amesema “Tunataka Abdul Nondo aachiwe mara moja akiwa mzma wa afya, tafadhali sana, gari inadaiwa parking na tumejua kila mahala gari hiyo inapaki, mwacheni Nondo haraka iwezekanavyo Wapumbavu wakubwa nyie”
Jeshi la Polisi limesema leo December 01,2024 majira ya saa 11.00 alfajiri katika eneo la stendi ya Magufuli Mbezi Louis Dar es salaam kuna Mtu mmoja Mwanaume amekamatwa kwa nguvu na kuchukuliwa na Watu waliokuwa wakitumia gari lenye usajili wa namba T 249 CMV aina ya Landcruiser rangi nyeupe na kwamba ilielezwa na Mashuhuda kuwa katika purukushani za ukamataji begi dogo lilidondoshwa na baaadhi ya vitu vilivyokuwemo vimetambuliwa ni vya Abdul Omary Nondo.
Msemaji wa Polisi, David Misime amesema “Ufuatiliaji wa tukio hilo ulianza mara tu baada ya kupokelewa kwa taarifa hiyo Polisi, sambamba na kufungua jalada”