LGE2024 Zitto: Vijana msiruhusu wasiokuwa wakazi kupiga kura Mwandiga

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Kiongozi mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, amewataka vijana wa Mwandiga, mkoani Kigoma kuhakikisha wanapiga doria katika eneo lao siku ya uchaguzi ili kuzuia mtu yeyote asiyekuwa mkazi wa eneo hilo kupiga kura.

Kupata taarifa na matukio ya kimkoa kuhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Akihutubia wananchi wa mtaa wa Kibingo, katika mamlaka ya mji mdogo wa Mwandiga, Wilaya ya Kigoma, Novemba 25, 2024, Zitto amesema hatua hiyo ni muhimu kwa kulinda haki ya wananchi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.

"Tunataka kila kura iheshimiwe, na mtu asiyekuwa mkazi wa Kibingo asiwe na nafasi ya kushiriki katika uchaguzi huu," amesema Zitto.

Zitto pia amewataka mawakala wa chama hicho kuhakikisha wanazilinda kura dhidi ya vitendo vya ubadhirifu, huku akitoa onyo kali kwa wasimamizi wa uchaguzi.

"Hapa Kigoma haitatokea msimamizi wa uchaguzi kubadili matokeo. Tumejipanga kuhakikisha haki inatendeka na tutashughulika na wasimamizi wa aina hiyo mmoja mmoja," amesema kwa msisitizo.

Aidha, amewahamasisha wakazi wa Mwandiga kutoruhusu mtu mwingine kuwachagulia viongozi wa kuwatumikia kwa miaka mitano ijayo.

"Wananchi wanastahili haki ya kupata uongozi bora. Msimkubalie mtu mmoja awaamulie hatma ya maisha yenu," ameongeza.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa umepangwa kufanyika nchi nzima Novemba 27, 2024, na vyama vya siasa vinaendelea na kampeni kwa lengo la kuhamasisha wananchi kushiriki na kupigia kura wagombea wao.
 
Wakuu,

Kiongozi mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, amewataka vijana wa Mwandiga, mkoani Kigoma kuhakikisha wanapiga doria katika eneo lao siku ya uchaguzi ili kuzuia mtu yeyote asiyekuwa mkazi wa eneo hilo kupiga kura.

Akihutubia wananchi wa mtaa wa Kibingo, katika mamlaka ya mji mdogo wa Mwandiga, Wilaya ya Kigoma, Novemba 25, 2024, Zitto amesema hatua hiyo ni muhimu kwa kulinda haki ya wananchi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.

"Tunataka kila kura iheshimiwe, na mtu asiyekuwa mkazi wa Kibingo asiwe na nafasi ya kushiriki katika uchaguzi huu," amesema Zitto.

Zitto pia amewataka mawakala wa chama hicho kuhakikisha wanazilinda kura dhidi ya vitendo vya ubadhirifu, huku akitoa onyo kali kwa wasimamizi wa uchaguzi.

"Hapa Kigoma haitatokea msimamizi wa uchaguzi kubadili matokeo. Tumejipanga kuhakikisha haki inatendeka na tutashughulika na wasimamizi wa aina hiyo mmoja mmoja," amesema kwa msisitizo.

Aidha, amewahamasisha wakazi wa Mwandiga kutoruhusu mtu mwingine kuwachagulia viongozi wa kuwatumikia kwa miaka mitano ijayo.

"Wananchi wanastahili haki ya kupata uongozi bora. Msimkubalie mtu mmoja awaamulie hatma ya maisha yenu," ameongeza.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa umepangwa kufanyika nchi nzima Novemba 27, 2024, na vyama vya siasa vinaendelea na kampeni kwa lengo la kuhamasisha wananchi kushiriki na kupigia kura wagombea wao.
Ni muhimu vijanaa hao kujiepusha kuingilia kazi na majukumu ya watu wengine kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi.

Wazururaji usiku au mchana kwenye maeneo vilipo vituo vya kupigia kura watakamatwa na kuwajibishwa ili kuimarisha amani kwa ajili ya wenye haki ya kupiga kura.

Fujo za uchaguzi zisikufanye ulale korokoroni ukiwa na maumivu makali ya virungu 🐒
 
Katika watu nao wadhalau humu jf wewe number moja
 
Back
Top Bottom