Uchaguzi 2020 Zitto Zuberi Kabwe: Hakuna Jimbo lolote la Lindi ambalo Chama cha Mapinduzi (CCM) kitashinda

Uchaguzi 2020 Zitto Zuberi Kabwe: Hakuna Jimbo lolote la Lindi ambalo Chama cha Mapinduzi (CCM) kitashinda

MOSintel Inc

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2016
Posts
817
Reaction score
593
Wasalaam wanabodi,

Poleni sana na majukumu ya kuijenga nchi yetu pendwa Tanzania.

Akiongea na waandishi wa habari, kiongozi wa chama cha ACT-WAZALENDO ndg. Zitto Zuberi Kabwe baada ya kuulizwa maoni yake juu ya kauli ya ndg. Nape Nnauye aliyoisema siku chache zilizopita, ndg. Zitto alikuwa ana haya ya kusema:

Kuhusu kauli ya ndugu yangu na rafiki yangu Nape Nnauye; Mimi ile kauli naiona ni panic; Kwasababu Nape anafahamu mazingira ya Jimbo la Mtama. Kwahiyo ni hali ya kawaida tu, kuona ni panic; Kwahiyo naamini kabisa ile ni kauli ya panic haina maana yoyote"

Ni kauli ambayo kwetu sisi wala haitusumbui, mtu anapokuwa kwenye wasiwasi wa kwamba Jimbo linaondoka anaweza sema lolote lile. Na ndugu yangu rafiki yangu Nape anajua kwamba hakuna Jimbo lolote la mkoa wa Lindi ambalo CCM watashinda hata Jimbo moja.

Mimi nimekwenda na nimetembea majimbo yote ya mkoa wa lindi, mwezi wa saba na mwezi huu wa nane. Sijaacha hata Jimbo moja. Hakuna jimbo Chama cha Mapinduzi watashinda Lindi, ndio maana mnaona matukio ya utekaji.

Haya yanafanyika ili kuzuia wagombea wasigombee, maana sio watu wa ACT tu walitekwa mwezi huu, Kuna mgombea wa CHADEMA ametekwa na yeye na kupigwa. Kwahiyo lengo lao ni kuhakikisha kwamba, pale RUANGWA hakuna mgombea(wa upinzani) kabisa.

Mimi sina cha kumwambia ndugu yangu Nape, naelewa kwenye siasa kunakuwa na panic, unaweza sema chochote. Mimi nimemsamehe tu. Sisi wala hatutamchokoza mtu. Sisi tunakwenda kushinda, tunakwenda kuchukua majimbo ili kuijenga Tanzania ambayo watu wana HAKI, wanna DEMOKRASIA, wanna UHURU ambayo huduma za kijamii Bora na za ufanisi zina patikana kwa wananchi na ambayo inajenga UCHUMI wa watu na sio uchumi wa serikali.

MY TAKE: Jimbo la RUANGWA ni kwa ndugu Kassim Majaliwa, huyu Zitto anajiamini vipi kutoa kauli hii kuelekea uchaguzi mkuu?

Nini maoni yako?
 
Kwani hao inavyosemekana wametakiwa, Je! Bado wapo chini ya watekaji au wameshaachiliwa? Na fomu wameshachukua? Na kama wanazofomu watazirudisha ili waingie kwenye mchakato wa kugombea?
 
Nakubaliana na wewe kuwa watu hawaipendi ccm kisa mateso wanayo endelea kuyapata, ila kuna sehemu ni vigumu kuyapata kutokana na wabunge waliopo
Wabunge wanapiga kura au wananchi?
 
Zitto anajaribu kutengeneza namna kuwaaminisha chadema kuwa act inakubalika pia bara so iwe rahisi kuwashawishi kumuachia baadhi ya maeneo wakati wa kuachiana maeneo ya kugombea. Kwamba ccm haishindi jimbo hata moja Lindi nadhani kwa mawazo haya zitto yuko katika hatua za awali za kuwa kichaa
 
Back
Top Bottom