Zitungwe sheria kuweka mipaka ya utani kwenye soka letu hasa timu za simba na yanga,na wachambuzi wawekewe mipaka yao

kambale mnene

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2022
Posts
271
Reaction score
197
Miaka ya Mimi nikiwa kijana utani wa simba na yanga ulikuwa wa kucheka na kufurahi.SOKA LILIKUWA TAMU

Miaka hii,imekuwa robo tatu ni vita,chuki ugomvi na kudharaulina.
Hii hali ikiachwa iendelee haitatutoa kwenye unyonge wa soka barani afrika na duniani kwa ujumla

Ni muda sasa wizara husika kuweka mipaka ya utani kwa kupeleka muswada bungeni ili utani uwe na mipaka.
Wanaijiita wachambuzi,nao wamekuwa wachonganishi sana,baina ya mtu na mtu,club na club

Utakuta tukio dogo sana ( tofauti) baina ya mtu na mtu,lakini wanavyolikuza huwezi amini kuwa hao ndiyo wanaopiga kelele juu ya soka letu kudorola.

Badala ya kuchambua choka waenda kuchambua tofauti za watu.
Hata kama mkosewa alitaka kusamehe anakolezwa moto.
SOKA LETU LISIMAMIWE KISHERIA
 
miaka hiyo kila mtu alikuwa na ajira ya uhakika ya kujiingizia kipato,siku hizi hata kuhamasisha wapenzi wa timu fulani waende uwanjani,tayari ni ajira ya kuendesha familia,inabidi utukane sana tena kwa bidii timu pinzani ili muamala usome,hilo ndio soka la bongo...
 
Tuanze na mambumbu fc wanaojiita mabingwa wa kihistoria tukiona wanaenda airport tuwapige mawe na yule nguruwe pori wao afungiwe maana anadhalilisha watu hapo amani itapatikana maana juzi walipochukua ubingwa yule mke wa mzee tozi akawashauri wakashangilie ubingwa karibu na jengo la msimbazi ili waone nini kitatokea ila wao Arusha walimpiga mtu mpaka akafa kisa kavaa jezi ya simba kwa hyo Yanga watungie sheria maana hawajielewi sio wanangu wa msimbazi.
 
Ukisoma comments za mtu mmoja huko juu utaelewa kwanini huu utani wa Simba na Yanga ni ngumu kutoka kwenye vichwa vyao
 
Mbona mbumbumbu ni makolo au mambo yamegeuka
 
Hakuna haja Ya Kuweka Mipaka Wala Minyau...! Wakati Kuna timu mojawapo Msemaji Wao alisha waambia Wooote ni Hamnazo Na Hawana Akili isipokuwa Baba yake Na Mzee Wa Msoga... Sasa unataniana nini Na punguani.!
 
Ila huyu mzee Rage akamatwe achunguzwe maana ile kauli yake inaishi, atakua ni 'genius' huyu
 
Hakuna haja Ya Kuweka Mipaka Wala Minyau...! Wakati Kuna timu mojawapo Msemaji Wao alisha waambia Wooote ni Hamnazo Na Hawana Akili isipokuwa Baba yake Na Mzee Wa Msoga... Sasa unataniana nini Na punguani.!
Na alisema kufanya kazi pale labda maiti yake, na sahivi ndo maiti iko huko inafanya kazi, sasa nani atakua na utani na Maiti?

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23], waelezee waeleze
 
Unachukia watu bure huo ugumu wa maisha unaopitia utoke kwa jina la Yesu sema Amen

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Wewe kweli taahira mbumbumbu fc huwajui mpaka sasa?? Yanga unawaita mbumbumbu fc wakati hili ni jina lenu pendwa mlipewa na Alhaj Aden Rage?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…