Ziwa Basotu, wilaya ya Hanang, mkoa wa Manyara lilishafanyiwa maboresho?

Ziwa Basotu, wilaya ya Hanang, mkoa wa Manyara lilishafanyiwa maboresho?

Idrissou02

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2018
Posts
354
Reaction score
656
Mnamo mwaka 2020 kuelekea mpaka 2021, ziwa Basotu, wilaya ya Hanang, mkoani Manyara lilikuwa linaleta madhara makubwa kwa wananchi kwa maji yake kujaa, kusambaa kwenye makazi ya watu na kusababisha mafuriko.

Nakumbuka vyombo vya habari vilitoa takwimu mwaka 2021 kuwa watu zaidi ya 90 walikosa makazi yaliyoezuliwa na maji yaliyotoka ziwa Basotu. Isitoshe, nakumbuka barabara maarufu iliyokua inaonganisha maeneo muhimu ilifungwa kwasababu ya maji kujaa na kuharibu miundombinu.

Naombeni mchango wenu kwa wakazi wa eneo husika au mtu mwingine yoyote anayefahamu kuwa ziwa lile lilishafanyiwa maboresho? Na je, maboresho hayo yameleta tija kwa wananchi au bado wananchi wa Hanang wanataseka?

Karibuni.
 
Hakuna maboresho yaliyofanyika, zaidi waliopata madhara makubwa wamesogea/wamehama. Mtu wa mwisho ni Mama Rose Kamili ambaye maji nayo hayamfii kutokana na upungufu mkubwa wa maji ziwani. Sasa hivi tunalia mvua hakuna mwaka wa tatu sasa, hata wale Kambale wakubwa hawapatikani tena.

Karibu sana Basotu tule nyama ya Boko (Kiboko)

photo_2022-10-10_11-36-25.jpg
 
View attachment 2382476
Poleni kwa changamoto. Kwaiyo ina maana watu waliokua wanategemea uvuvi wa samaki, wamekuwa wakipata faida ndogo kuliko kipindi cha nyuma?

Na kama ndio, je wananchi wa basotu wakiletewa mradi wa ufugaji wa samaki kwa kuchimba mabwawa watakua tiari kuupokea ili waondokane na adha iliyowakumba?
 
Back
Top Bottom