KWELI Ziwa Natron haligeuzi wanyama wanaokunywa au kuogelea maji yake kuwa Mawe bali huwakausha na kuhifadhi mizoga hiyo bila kuharibika

KWELI Ziwa Natron haligeuzi wanyama wanaokunywa au kuogelea maji yake kuwa Mawe bali huwakausha na kuhifadhi mizoga hiyo bila kuharibika

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Je, ni kweli Ziwa Natron linawageuza wanyama wanaokwenda kuogelea ndani yake kuwa mawe?

1734410797797.png
 
Tunachokijua
Ziwa Natron ni ziwa la chumvi au alkali ambalo linapatikana Kaskazini mwa Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha Tanzania na linapakana na Kenya kwa upande wa kusini. Lina mwinuko wa mita 600, ziwa linapata maji kutoka mto Ewaso Nyiro(ng'iro) ambao unatoka katikati mwa Kenya unaotoka kwenye chemchemi za maji moto zenye madini.

Lina kina kifupi sana, chini ya mita tatu(futi 10) na maeneo ya ziwa hutofautiana kina kulingana na kiwango cha maji. Lina urefu wa juu wa kilomita 57 na upana wa kilomita 22.

462188239_2555647181286913_8886635979371786597_n.jpg
Kumekuwapo na Madai kuwa Ziwa Natron lina uwezo wa kuwageuza kuwa mawe wanyama na ndege wanaokunywa au kuogelea kwenye maji yake

Je, ni upi uhalisia wake?

JamiiCheck imepitia machapisho na Tafiti mbali mbali na kubaini kuwa Ziwa Natron Haligeuzi Wanyama na ndege kuwa Mawe bali wakifa hukauka na kuzingirwa na chumvi na hivyo kubaki katika hali hiyo kwa kuwa mazingira ya Ziwa Natron hayaruhusu ukuaji wa Bakteria wanaoweza kuishambulia ili ioze.

Kwa mujibu wa LiveScience Ziwa Natron lina kiwango cha juu sana cha alkali, ikiwa na PH ya 10.5 na wakati mwingine huzidi hadi 12 au zaidi kutokana na uwepo wa madini ya sodium carbonate na magnesiamu pamoja na madinimengine yanayotoka kwenye mlima wenye volkano. Aidha, maji yake yana joto ambalo linaweza kufikia hadi nyuzi joto 60°C, na uwepo wa chumvi nyingi kwenye Ziwa hufanya mazingira yasiyoweza kuhimiliwa na ndege au wanyama ambao hawajazoea hali hiyo wakiogelea na kuyanywa maji hayo kwa wingi hufa.

Mchanganyiko wa alikali na joto kali huua viumbe wanaoingia majini. Baada ya kufa, miili yao huhifadhiwa kwa sababu ya kuwepo kwa madini ya Sodium carbonate kwenye Ziwa hilo, Sodium carbonate yalitumika katika utunzaji wa mabaki ya wanyama wa kale (mummification), huzuia kuoza kwa miili. Wanyama wanaokufa ndani au karibu na ziwa huhifadhiwa vizuri, Wakiwa wamezingirwa na chumvi nyingi hali ambayo hutafsiriwa kama wamegeuzwa kuwa mawe ila Si kweli kama hugeuzwa Mawe bali hubaki katika hali ya kukauka.

Miamba inayolizunguka ziwa hili imeundwa na miamba ya trachyte yenye alikali, ambayo ina kiasi kikubwa cha sodium, lava inayopatikana katika eneo hili ina kiasi kikubwa cha carbonate lakini kiwango kidogo cha calcium na magnesiamu, hali hii imefanya ziwa hili kuwa na maji yenye alikali kali yenye sumu. Eneo hili lina lava kutokana na Ziwa kuwa karibu na Mlima Oldonyo Lengai ambao una Volkano

Ziwa hili linakumbwa na uvukizi mkubwa wa maji, jambo ambalo linaacha mkusanyiko mkubwa wa chumvi na madini mengine. Ziwa Natron linatofautiana sana na maziwa mengine ya chumvi kama Bahari ya Chumvi (Dead Sea) na Ziwa Kuu la Chumvi la Utah.
flamingo-lakes-2-two-column.jpg.thumb.768.768.jpg
Tofauti hii inatokana na wingi wa kemikali ya natron, ambayo ni mchanganyiko wa sodium carbonate na baking soda katika maji ya ziwa hili. Ziwa Natron halina mto wa kutiririsha maji nje, njia pekee ya maji kutoka ziwani ni kupitia uvukizi. Wakati wa msimu wa ukame, maji yanapovukizwa, kiwango cha chumvi katika ziwa huongezeka, na kuvutia viumbe (bakteria)wanaopenda chumvi ambao huanza kustawi. Viumbe hawa, wanaoitwa halofili, ni pamoja na cyanobacteria ambao hufanya rangi ya ziwa kuwa Nyekundu, machungwa au Pink, viumbe hawa hutengeneza chakula chao kwa njia ya usanisinuru (photosynthesis)

Hivyo, rangi ya ziwa hili inatokana na mwingiliano wa viumbe hai (bakteria na algae) pamoja na hali ya kijiografia na kemikali ya ziwa hilo. Rangi yake huweza kubadilika kulingana na msimu, kiwango cha maji, na hali ya joto.

New Scientist wanaeleza kuwa Ziwa Natron limepata sifa ya kuangamiza wanyama wanapoogelea katika maji yake ambayo yana chumvi nyingi sana na madini ya alkali sumu ambayo huweza kuunguza ngozi, kuharibu macho na kuwaua kabisa iwapo wakinywa maji yake kutokana na viwango vya juu vya bicarbonate ya sodiamu hukauka na kuhifadhiwa. Bicarbonate ya sodiamu ilitumiwa kihistoria na Wamisri kwa ajili ya mummification.
flamingo-lakes-3-two-column.jpg.thumb.768.768.jpg

Imeripotiwa kwamba ziwa hilo “hugeuza wanyama kuwa mawe wanapogusa wanapogusa au kuogelea” Hata hivyo, wanyama hao hawakufa kwa sababu waligusa maji ya ziwa hilo. Wanyama hao walikufa majini kwa sababu ya kunywa maji ambayo yana chumvi kali na alkali na mizoga yao ikahifadhiwa na kemikali zilizokuwa majini, hivyo kuwafanya kuwa sanamu za chumvi na si mawe kama inavyodaiwa.
mg21929360.100-2_800.jpg
Licha ya mazingira ya alikali nyingi na hali ngumu Ziwani, viumbe kama Flamingo wa Lesser, Samaki aina ya Tilapia na Mwani wa kijani na wa buluu vinaishi na kustawi humo

flamingo-lakes-full-width.jpg.thumb.1160.1160.jpg

Back
Top Bottom