Zoezi la kuapisha wajumbe wa bunge maalumu limekosewa

mandago shululu

Senior Member
Joined
Mar 24, 2013
Posts
125
Reaction score
36
Zoezi la kuapisha wajumbe wa katiba pamoja na wabunge-wajumbe la katiba linaloendele sasa linaendelea vizuri ila tu kwa wabunge-wajumbe namna wanavoopa wameshakosea.sana,wenyewe tayali ni wabunge wa kuchaguliwa wengine wakuteuliwa ambao wanakuwa na sifa ya kuwa wajumbe wa bunge maalumu la katiba.kwa sasa wanaapa kama ifuatavyo.
Mimi Martin W Mandago,niliyeteuliwa kuwa mjumbe wa bunge maalumu,ninaapa kwamba nitakuwa mwaminifu na mtiifu wa jumhuri ya muunganano wa Tanzania na kwa kadri ya uwezo na ufahamu wangu nitatimiza wajibu wangu na kufanya kazi zinazonihusu bila upendeleo,ewe mwenyezi mungu naomba unisaidie.
Kiapo hiki kinawafaa tu wale walioteuliwa kuwa wajumbe yaani kundi la 201 kama wanavyojiita wenyewe.Walikuwa wanapaswa kuapa kama ifuatavyo.
Mimi Martin W Mandago mbunge na mjumbe wa bunge maalumu------------.Kwa namna hiyo ingewafaa sana,naomba kutoa hoja.
Mandago 2015 kwimba@
 
Last edited by a moderator:
Wazo zuri.
Kimsingi wote ni wajumbe wenye hadhi sawa. Hilo ni Bunge Maalum la Katiba.
Wangeepa hivi;"Mimi.......... mjumbe/mbunge wa bunge maalum la katiba........ ".
 
Mkuu, hakika wewe ndo unajichanganya. Kwanza ujue kuwa hakuna uchaguzi ulifanyika kwa ajili ya wabunge wa Bunge Maalum. Wabunge wote wa bunge hili ni wa kuteuliwa. Katika kurahisisha uteuzi huo, kuna makundi matatu. Yaani kundi la wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania, wajumbe wa baraza la wawakilishi na wale 201. Wabunge wote 629 wamepewa barua za uteuzi kufanya kazi kwenye bunge maalum na ndo maana unaona wanaapishwa hata wale ambaoni wabunge tayari. Kwa concept yako, hakukuwa na haja ya hawa wengine kuapa
 
Sidhani kama Mh. Lissu alishirikishwa kuandaa hicho kiapo. Sana sana kitakuwa kiliandaliwa na "mfuga manywele" na timu yake; wazee wa kuchemka.
 
Mkuu, hicho kiapo kimeandaliwa na akamati ya Kanuni na Lissu ni mjumbe mmoja wapo
 
Kinacho nishitua mimi ni uwingi wawanao shika kuran,Mbona wengi sana,yaani kama robotatu ivi.Kusije kukawa na mpango wa mahakama ya kadhi!
 
Masuala ya wingi ya wanaoshika kur-an yanatokea wapi? ulitaka wa bible ndiyo wawe wengi? acha mawazo mgando! 201 wameteuliwa kwa uwiano ulio sawa!
 
Kinacho nishitua mimi ni uwingi wawanao shika kuran,Mbona wengi sana,yaani kama robotatu ivi.Kusije kukawa na mpango wa mahakama ya kadhi!

nini kinakuogopesha sasa...kushika au wingi wao au kutaka kadhi...?
 
Kinacho nishitua mimi ni uwingi wawanao shika kuran,Mbona wengi sana,yaani kama robotatu ivi.Kusije kukawa na mpango wa mahakama ya kadhi!

Teh teh teh! Pole rafiki naona unapata kumbukumbu za tindikali na mabomu! Karibu kwetu Nigeria!
 
Kinacho nishitua mimi ni uwingi wawanao shika kuran,Mbona wengi sana,yaani kama robotatu ivi.Kusije kukawa na mpango wa mahakama ya kadhi!

Unaogopa nini Kijana, waache wahukumiane. Au unafikiri Boko Haram wamejipenyeza?
 
Zoezi la kuapisha wajumbe wa katiba pamoja na wabunge-wajumbe la katiba linaloendele sasa linaendelea vizuri ila tu kwa wabunge-wajumbe namna wanavoopa wameshakosea.sana,wenyewe tayali ni wabunge wa kuchaguliwa wengine wakuteuliwa ambao wanakuwa na sifa ya kuwa wajumbe wa bunge maalumu la katiba.kwa sasa wanaapa kama ifuatavyo.
Mimi Martin W Mandago,niliyeteuliwa kuwa mjumbe wa bunge maalumu,ninaapa kwamba nitakuwa mwaminifu na mtiifu wa jumhuri ya muunganano wa Tanzania na kwa kadri ya uwezo na ufahamu wangu nitatimiza wajibu wangu na kufanya kazi zinazonihusu bila upendeleo,ewe mwenyezi mungu naomba unisaidie.
Kiapo hiki kinawafaa tu wale walioteuliwa kuwa wajumbe yaani kundi la 201 kama wanavyojiita wenyewe.Walikuwa wanapaswa kuapa kama ifuatavyo.
Mimi Martin W Mandago mbunge na mjumbe wa bunge maalumu------------.Kwa namna hiyo ingewafaa sana,naomba kutoa hoja.
Mandago 2015 kwimba@

Uteuzi wao kwa ujumla ulizingatia makundi hayo 3. Hivyo kwa kuwa tu tayari mbunge wa bunge la Jamuhuri au wawakilishi tayari umeteuliwa kutokana na nafasi uliyopo. Kumbuka kati yao wote hakuna aliyechaguliwa na wananchi kwa ajili ya bunge maalum la katiba. Baada ya Rais kuona katiba mpya ni muhimu, basi wateule wa kwanza ndo hao.
 
Last edited by a moderator:
Sidhani kama Mh. Lissu alishirikishwa kuandaa hicho kiapo. Sana sana kitakuwa kiliandaliwa na "mfuga manywele" na timu yake; wazee wa kuchemka.

Lissu ndio nani katika taifa hili?
 
mkuu lile ni bunge la katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania wala sio mkusanyiko wakigango fulani cha kanisa fulani sehemu hulani. badilika tusonge mbele. kama unahitaji mkusanyiko wa wakristo nenda kesho kanisani, ni jumapili.

Back
Top Bottom