Pre GE2025 Zoezi la kujiandikisha daftari la Mpiga Kura Mtwara kuanza Februari 27, 2025

Pre GE2025 Zoezi la kujiandikisha daftari la Mpiga Kura Mtwara kuanza Februari 27, 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mabalozi wa CCM wilaya ya Mtwara Mjini wametakiwa kuhamasisha wananchi, hasa vijana, mama lishe, na wanachama wasiokuwa na vitambulisho vya mpiga kura, kushiriki kwenye zoezi la kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura linalotarajiwa kufanyika Februari 27, 2025.

Soma, Pia: Afisa Uandikishaji Halmashauri ya Mbeya: Msilewe na kutumia vilevi wakati mnaandikisha wananchi kwenye daftari la kudumu la wapiga kura

Katibu wa CCM wilaya hiyo, Fadhiri Mrami, alieleza kuwa Manispaa ya Mtwara Mikindani ina wakazi 145,536, kati yao wanachama wa CCM ni 33,420, akisisitiza umuhimu wa kuongeza wanachama.

Mbunge wa Mtwara Mjini, Hassan Mtenga, alitumia kikao hicho kufikisha salamu za Rais Samia na kuahidi mifuko 100 ya saruji kwa kata 17 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za chama.

Mwenyekiti wa Mabalozi Kata ya Likombe, Muhammed Milanzi, alisisitiza mabalozi kutanguliza maslahi ya wananchi katika uchaguzi mkuu.
IMG_2276.jpeg
 
Back
Top Bottom