The Burning Spear
JF-Expert Member
- Dec 23, 2011
- 4,118
- 9,864
Let's now be serious from jokes, at least for a moment.
Bila shaka kila mmoja anafahamu kuwa kuna uchaguzi wa serikali za mitaa unakuja mwezi novemba 2024.
Baada ya hamasa kubwa kupitia vyombo mbalimbali na media na hata matangazo ya mtaa kwa mtaa, juzi nilijisogeza hadi kwenye kituo cha kujiandikisha kwa ajili ya kupiga kura.
Nilipofika niliwakuta watu watatu mmoja alikuwa anayeandikisha wapiga kura na wawili walioketi pembeni ni mawakala wa vyama
Baada ya salaam nikaket ili kupata maelekezo ya kujiandikisha.
Maswali yalikuwa matatu tu.
1. Taja majina yako matatu
2. Unaishi au wewe ni mkazi wa eneo hili ?
3. Umri wako ni miaka mingapi?
Basi hayo tu.
Hawakuniuliza hata kitambulisho changu chochote. Ila majina matatu!
1. Kwa ajili ya consistency nikatoa kitambulisho changu cha mpiga kura (ili majina yasije tofautiana).
2. Yule kijana akauliza kama mimi ni mkazi wa eneo hilo.
3. Akauliza umri wangu.
Nilipigwa na butwaa na simplicity ya uandikishaji. Sikutarajia iwe rahisi hivyo.
Sikuweza kuvumulia bila kuuliza maswali.
Hivi, kwanini mwandikishaji hakuniuliza ninaishi mtaa gani na nyumba namba ngapi?
Kitambulisho changu
Mwandikishaji anatafiti kitu gani kuthibitisha kama mimi ni eligible kujiandikisha kwa ajili ya kupiga kura?
Kama sikuulizwa kitambulisho,
Sikuulizwa anwani ya makazi,
Sikuulizwa kutoa uthibitisho mwingine wowote kuwa mimi ni mkazi wa eneo hilo,
Je, kwa maswali mengine kama mimi ni raia itakuwaje?
Mwandikishaji alijitahidi kujibu na kunitoa wasiwasi kuwa
Uandikishaji unafanyika kukiwa na observers ambao ni mawakala wa vyama. Hatua ya uandikishaji ni ya awali, itafuatiwa na hatua ya uhakiki kwa maana ya fursa ya kuweka pingamizi dhidi ya wanaodhaniwa hawana sifa ya kupiga kura!
Nikajiuliza kwa nini kuwe na mlolongo huo mrefu wa kusubiri uhakiki wakati ambapo chujio lingeweza kuwekwa mapema kwa kupata vithibitisho vya uhalali wa mpiga kura mtarajiwa?
Nikawaza waendesha mchakato nao wanahitaji posho ndiyo maana mtiririko unakuwa mrefu. Ukiondoa hatua moja maana yake unakata posho.
Mhh? Kwa maoni yangu ikiwa huu ndiyo mchakato wa kupata wapiga kura, there is a lot to be desired. Hapa hakuna kitu. Ila mianya ya kuvuruga mchakato wa kura iwe kwa kujua au kutokujua huko ndiko tunakoelekea.
Mtu anayeweza kumtambua mkazi wa eneo au mtaa kama si mwenyekiti wa mtaa, au kitongoji na pia mjumbe wa nyumba kumi ni nani mwingine.
Kwa kawaida mtu ukitaka huduma mbalimbali kama za kiserikali au benki nk. Utambulisho maalum unahitajika kutoka serikali ya mtaa. Iweje katika jambo muhimu kama la uchaguzi hakuna machujio kama haya?
Huu mfumo ndiyo umeshakuwa designed. Si bahati mbaya au kwa makosa. Walioubuni wana uhakika na unavyofanya kazi.
Let's wait and see.