KERO Zoezi la uboreshaji wa taarifa za NMB Mwanza limekosa umakini na weledi

KERO Zoezi la uboreshaji wa taarifa za NMB Mwanza limekosa umakini na weledi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Nikiwa mkazi wa mwanza na mdau wa bank ya NMB sijaridhishwa na zoezi linaloendelea la kuboresha taarifa za wateja wa bank hii.

Tangu mwezi wa 7 bank ya NMB katika matawi yake ya Mwanza imekua ikiboresha taarifa za wateja wake ila zoezi ili limekua bovu na lisoloendana na kasi ya tenkolojia wala kulinda faragha za wateja kutokana na linavoendeshwa kama ifuatavyo;

1. Inabidi wateja tuache kazi zetu kwenda bank kuboresha taarifa ambapo tunakutana na foleni kubwa katika kuboresha taarifa.Kwa nn NMB wasingeweka utaratibu rafiki kwa wateja kuboresha taarifa bila kupanga foleni wala kuja bank physically.Yako wapi matumizi ya teknolojia?kwa nn wateja tusingepewa link ya kuboresha taarifa zetu online?

2. Fomu anayojaza mteja wakati wa uboreshaji imeandikwa kwa kiingereza tena kile kiingereza cha kisheria?je wateja wanajua wanaingia makubaliano gani na bank kwa kusaini fomu ambayo hawajui kilichoandikwa ndani.Na kiuhalisia wateja wengi hawasomi kile kilichoandikwa bali wanaambiwa tu kujaza majina na kuweka sahini zao.

3. Usalama wa taarifa za mteja upo mashakani maana mteja anaulizwa taarifa zake binafsi kama namba ya simu,kazi na kipato chake kwa mwezi uku pembeni yake kuna wateja wanaofatia kwenye foleni wanasikiliza taarifa za mteja mwenzao sababu hakuna privacy kabisa

Kiufupi zoezi ili linaendeshwa kizamani sana kama vile hatuna teknolojia na linatuingiza wateja katika gharama zisizokua na msingi ikiwemo kupotezewa muda na wakati mwingine pesa kwa kwenda mahakamani au kwa mwanasheria ili kuhakiki majina.

Napenda kushauri uongozi wa NMB waipe kipaumbele teknolojia katika jambo ili,kama mteja naweza kufanya online transactions kweli nitashindwa kufanya obereshaji online?

F4964571-4321-45CB-A675-BB6D58F6956D.jpeg
 
Back
Top Bottom