Zoezi la ugawaji sanitizer bure laanza

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368

Kampuni ya Usafirishaji wa Mafuta nchini Kenya -- The Kenya Pipeline Company (KPC), ikishirikiana na wadau kadhaa wa sekta binafsi na ya umma wamechangia kiasi cha lita 130,000 za sanitizer zinazotolewa bure kwa wananchi ikiwa ni juhudi katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona.

Sanitizer hizo zinatolewa kwenye chupa za mililita 500 kwa matumizi ya kaya mojamoja na katika vyombo vya lita 20 kwa taasisi kama vile vituo vya afya, vituo vya polisi na katika masoko.

"Katika kipindi kisichozidi wiki mbili, KPC na wadau wengine wamezalisha zaidi ya lita 130,000 za sanitizer za bure ili kuwanufaisha watu walio hatarini zaidi kupata maambukizi nchini. Hii itasaidia kupunguza kuenea kwa COVID-19” Amesema Macharia Irungu, Mkurugenzi Mtendaji wa KPC

Mpango huu ni sehemu ya juhudi ya serikali kupunguza kuenea kwa COVID-19, ambapo katika barua iliyoandikwa Machi 18, 2020, Rais Uhuru Kenyatta aliitaka KPC kuratibu uzalishaji wa sanitizer na kusambazwa bure kwa wananchi, hususani wanoishi katika makazi yasiyo rasmi.

Hadi sasa, zaidi ya lita 93,000 tayari zimetolewa kwa kaunti za Nairobi, Kilifi, Mombasa, Kwale na Nakuru. Maeneo mengine ni pamoja na Siaya, Kajiado, Kiambu, Murang’a, Makueni na Machakos.

======

The Kenya Pipeline Company (KPC) has partnered with several private and public sector players to donate 130,000 litres of free hand sanitizers in the fight against coronavirus.

The sanitizers have been packed into 500ml bottles for household use and 20-litre containers for institutions such as health facilities, police stations, market centres.

“In less than two weeks, KPC, oil marketing companies and other players have produced over 130,000 litres of free hand sanitizers to benefit Kenya’s most vulnerable people. This will go a long way in mitigating the spread of COVID-19 in the country,” said KPC Managing Director Macharia Irungu.

The free hand sanitizers initiative is part of the government’s effort to curb the spread of COVID-19 in the country.

In a letter dated March 18, 2020, President Uhuru Kenyatta had tasked KPC to produce alcohol-based sanitizer for free distribution to the public.

Principal Secretary for Petroleum Andrew Kamau said the hand sanitizers, whose production KPC was coordinating, would be distributed for free across the country.

The main target is Kenyans living in informal settlements.

The sanitizers will be transported across the country by different partners including East African Breweries, Bollore Logistics, and Maersk Kenya.

KPC has also appealed to more State and non-State actors to support the initiative as it targets to produce more sanitizer in the coming weeks.

So far, over 93,000 litres of the free hand sanitizers have been released to several counties namely: Nairobi, Kilifi, Mombasa, Kwale and Nakuru. Others include Siaya, Kajiado, Kiambu, Muranga, Makueni and Machakos.

Source: Citizen TV
 
Jamaa wa Turkana mbona wanasahauliwa?
 
Wrong approach in combating COVID-19

Wanatakiwa kuhimiza watu wanawe kwa maji na sabuni ambayo n njia rahisi sana
 
Wrong approach in combating COVID-19

Wanatakiwa kuhimiza watu wanawe kwa maji na sabuni ambayo n njia rahisi sana

Watanzania sijui nani kawaroga mpaka mumekosa akili kiasi hiki, wewe unategemea maji na sabuni kote mpaka kwenye daladala????
Hand sanitizer husaidia kwenye maeneo ambapo hutegemei kupata maji na sabuni. Hauwezi ukaweka maji na sabuni kila mahali ila kwa hand sanitizer utaweka popote pale, na pia ukinyunyiza mikono hiyo ethanol hata ushike sehemu yenye kirusi kitakufa moja kwa moja, ila ukinawa kwa maji kisha ushike kirusi, kitabaki mikononi....
Shule zenu mnafundishwa ujinga.....@FaizaFoxy
 
Wrong approach in combating COVID-19

Wanatakiwa kuhimiza watu wanawe kwa maji na sabuni ambayo n njia rahisi sana
sasa shida iko wapi iwapo sabuni za kunawia mikono wanapewa bure???
uwe unaushirikisha ubongo wako sometimes ukija kwenye jukwaa hili,,, watu kama nyinyi ndio munaotufanya Wabongo tuzaraulike na Wakenya.
 
Pokot na Turkana ni kama wamesahauliwa vile.
kwani ulisikia Corona imefika Turkana? hapa tunadili na sehemu ambazo ziko prone kwanza na huu ndio mwanzo tu.
shirikisha ubongo wako japo kidogo tu kabla ya kukurupuka.
 
Safi sana, zipokezwe kote, kwa kweli serikali inajitahidi sana kuendelea kuwezesha Kenya kujichimbia kabla maangamizi hayajaja, tunayoyasoma kule Ulaya yanatisha balaa.
Acheni kupigana bakora mpaka wanawake chupi zinawavuka
Corona haiondoki kwa kupigana bakora
 
HA ha ha ha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…