Zoezi la ukusanyaji taka ambalo wanachaji Tshs 3,000 hadi 5,000 kila kaya bila kutoa risiti za kielektroniki lina baraka za mamlaka?

Zoezi la ukusanyaji taka ambalo wanachaji Tshs 3,000 hadi 5,000 kila kaya bila kutoa risiti za kielektroniki lina baraka za mamlaka?

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2018
Posts
2,490
Reaction score
3,584
Habari wadau,

Kwenye mitaa yetu hususa huku uswazi kuna zoezi la ukusanyaji taka ambalo wanachaji 3000/= mpaka 5000/= kila kaya kiukweli hii ni pesa nyingi sana ambayo serikali za mitaa/mkandarasi wa taka anakusanya cha ajabu ukilipa haupewi risiti ya electronic.

Ila point yangu ni:

Je, hili zoezi limepata baraka zote toka wizara husika na serikali kuu?

Je, Taifa halioni linapoteza mapato kupitia utaratibu huu wa ukusanyaji na utoaji wa risiti zisizo za electronic?

Je, ushirikishwaji wa wananchi kuhusu viwango vya kulipia ulifuatwa?

Asanteni
 
Wasiliana na diwani pamoja na mtendaji bila kusahahu mwenyekiti wa mtaa watakupa maelezo konki. Maoni yangu kama mtaa umeanza kuwa msafi haina shida, nataman hata huku wafanye hvo ili mtaa uwe Safi. Uchafu ni kero na kiukwel wanaosafisha inabd walipwe hela nzuri.
 
Uwazi kwenye malipo ni muhimu, unaweza kufikiria unawalipa vizuri kumbe pesa inaishia kwa diwani na watendaji wachache.
 
Maswali yangu umeyaona lakini au umekimbilia ku comment tu?
 
Uwazi kwenye malipo ni muhimu, unaweza kufikiria unawalipa vizuri kumbe pesa inaishia kwa diwani na watendaji wachache.
Umenena vyema,kitendo cha kutoa virisiti vya karatasi vilivyochapishwa mtaa wa gerezani vinatia shaka kwa kweli ,hata wananchi wanahoji utaratibu huu bila kupewa majibu.Tusije tukawa tunalikosesha Taifa mapato.
 
Usafi muhimu sana.
Dai stakabadhi ya EFD, mitaa mingi hapa Dar wanatoza bei hiyo hiyo na lazima wakupe hiyo kitu ya EFD kupitia zile mashine portable za POS.
 
Hawa watu wanafanya kazi muhimu ila hakuna uwazi na pia utakuta kwa week wanapita mara moja na wanataka huku 5, sasa kwa kupita mara moja kwa week, hudumu yao ni muhimu ila ubora wa huduma zao ni hafifu.
 
Baada ya mabeberu kukaza na pesa yao, Sirro ameagizwa ukusanyaji wa makosa ya barabarani ni lazima uongezeke. Kumbe na madiwani pia wamepewawmaelekezo.
TARURA, tra, traffic, Halmashauri, Nemc, TMDA, Serkali za mitaa, TCRA wote wanakusanya mapato
 
Maswali yangu umeyaona lakini au umekimbilia ku comment tu?
Maswali yako nimeyaona, na hakuna wa kuweza kuyajibu humu labda awe kiongozi husika wa mtaani kwako, kwa sababu hzo tozo zipo chini ya serikali za mitaa hivyo madiwani, watendaji na wenyeviti wa mtaa ndo wanahusika kawaone watakupa maelezo, kama wamekosea utaratibu ukawawashie huko huko. Hizo tozo hazifanani Tanzania nzima kuna mitaa mingine wanatoza 1000, mingine 500.
 
MITANO TENA

🤣🤣🤣

Anyway, labda nikusaidie kuelewa: Mimi ni afisa afya hizo pesa kazi yake inaishia tu ofisi za mtendahi wa mtaa.

Ni kwaajili ya malipo ya pisho kwa mtendaji, pesa Kidogo ya kuleta gari, kuwaoipa xhawa wa mwenyekiti wanaokusanya pesa, afisa afya na diwani.

Hivyo kila mtaa wanahikusanyia pesa wanayoona inatosha.

Na ndiyo posho yao, hawana kazi nyingine ndio maana hata ukiwapa buku hawaachi🤣🤣🤣🤣

Halafu wote nchi nzima ni CCM.

Mitano Tena 🤣🤣🤣🤣🤣
Hebu jifunze kuandika vizuri, naona una hoja ,lakini kuna makosa ya kisarufi mengi tu.

Hebu tuliza mpira kiongozi.
 
Huko kwenye 'mitaa yenu' ni wapi?

Taja jina la mtaa kitongoji na kata tufahamu kwa uzuri.
Mimi naishi Kwa Aziz Ally, wanakusanya buku 3 kwa kila familia, kila mwezi. Possibly labda ndio anakaa huku.

Mwaka jana nilikuwa nakaa kwa Mombasa, Ukonga mchango ulikuwa mia 2 tu kwa kila familia kwa mwezi
 
Habari wadau,

Kwenye mitaa yetu hususa huku uswazi kuna zoezi la ukusanyaji taka ambalo wanachaji 3000/= mpaka 5000/= kila kaya kiukweli hii ni pesa nyingi sana ambayo serikali za mitaa/mkandarasi wa taka anakusanya cha ajabu ukilipa haupewi risiti ya electronic.

Ila point yangu ni:

Je, hili zoezi limepata baraka zote toka wizara husika na serikali kuu?

Je, Taifa halioni linapoteza mapato kupitia utaratibu huu wa ukusanyaji na utoaji wa risiti zisizo za electronic?

Je, ushirikishwaji wa wananchi kuhusu viwango vya kulipia ulifuatwa?

Asanteni

Majibu ya maswali yako ni haya.

Mwenye mamlaka ya kutowa tender hizo ni mkurugenzi wa Halmashauri na anaweza kukasimu madaraka kwa mtendaji kata na diwani wake.

Kimsingi risiti za kielectronic ndizo zinapaswa kutumika kote, kama hao hawatumii basi iko mushkeli.

Kuhusu ushirikiswaji wananchi hawajashirikishwa, lakini wananchi wenyewe hata mikutano ya mtaa ikiitishwa hawatoke, wanaohudhuria mikutano ni walewale wasiokuwa na hela za kunywa bia, wanywa pombe hawana muda wa kuhudhuria hiyo mikutano bali kuja kulalamika hapa JF.

Mimi huwa silalamiki tu hapa kwenye kata yangu diwani alinijibu utumbo nilimtandika kibao cha uhakika na mpaka leo ananiheshimu na hakwenda kushtaki Polisi.
 
Umenena vyema mkuu sisi huku mbezi tunalipa 10,000/=. Mitaa ni safi wala hatuna shida kabisa huwezi ona marundo ya takataka. Wapite mara moja, mara kumi ni none of our business, bali tunachotaka takataka zisiwepo mitaani. Full stop! Pia tunalipa 15,000/= kwa ajili ya ulinzi maisha yanaendelea!
Sijui ni kwa nini maskini siku zote ndio wanaojikweza huku watu wenye maisha bora wanaaply low profile?

Huwa sielewi aisee, ona mpumbavu fukara kama huyu.
 
Sijui ni kwa nini maskini siku zote ndio wanaojikweza huku watu wenye maisha bora wanaaply low profile?

Huwa sielewi aisee, ona mpumbavu fukara kama huyu.
Hao ndio wasiojua hata bei ya kilo ya unga .😂😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom