Habari wana JamiiForums,
Tumepokea malalamiko na maswali mengi sana kuhusu kwa nini hatuoneshi email address za waajiri ili wanaotafuta kazi watume maombi moja kwa moja. Wengine wanafikiria kuwa tunafanya hivyo maana tunataka / tunapata ‘Commission' kutoka kwa waajiri. Ni matumaini yetu maelekezo yafuatayo yatasaidia kuondoa utata uliopo.
Kwanza kabisa, ZoomTanzania
HATUTOZI kiasi chochote kile kwa ajili ya mtu kupost nafazi za kazi. Sisi tunatoa huduma hii
BURE KABISA kwa waajiri na wanaotafuta kazi. Karibu Listings zetu zote ni bure, isipokuwa
FEATURED BUSINESS LISTINGS [BUSINESS DIRECTORY LISTING], ambazo ni hiari kwa Biashara mbalimbali. Mapato makubwa ya ZoomTanzania yanatokana na kuuza nafasi za matangazo (banner ads) kwa makampuni mbalimbali. Mfano mzuri ni matangazo ya Tigo, Zantel, CFAO na mengine yaliyopo kwenye website yetu.
Pili, tunaficha email za waajiri kwa sababu hivyo ndivyo wanavyopenda waajiri wengi. Ieleweke kuwa, hatufichi email kwenye nafazi za kazi tu, bali post zote zinazowekwa kwenye website yetu. Hii ni kawaida kabisa kwa website nyingi zilizotengenezwa mahsusi kwa ajili ya kutafuta kazi sehemu nyingi ulimwenguni. Kama tutaziweka email address ili zionekane, basi tutakumbwa na tatizo kubwa la programs kama "
Spiders" na "
Crawlers" ambazo utembelea kurasa zote za website yoyote ile, na hata yetu au yako, ili "
kukusanya" email addresses ambazo zipo kwenye site hiyo. Ukipenda kupata taarifa zaidi juu ya suala hili waweza kujisomea mwenyewe kwenye link hii >
Spambot - Wikipedia, the free encyclopedia.
Baada ya email hizi kukusanywa, huwa zinauzwa kwa makampuni ambayo huzitumia email hizo kutuma SPAM zenye ujumbe kuhusu Viagra, Pornography na SCAM nyingine mbalimbali.
Kwa hiyo, tusingezificha email, ni waajiri wachache sana ndo wangekubali kupost nafasi za kazi kwenye website yetu, na sisi tusingekuwa na kazi nyingi za ku-review na kuwajulisha kila siku.
Mwisho kabisa, kumekuwa na malalamiko kuwa "attachments" hazifiki. Asilimia 99.999% ya email zote zinazotumwa kwa waajiri, huwa zinafika na attachments. Katika miezi 18 iliyopita na katika maelfu za nafasi za kazi zilizowekwa kwenye website yetu, tumepata malalamiko kutoka kwa waajiri 3 tu ambao walitutaarifu kuwa walikuwa hawapokei attachments. Hili si tatizo la system yetu, tatizo hili ni la ‘Security settings' za email ya mwajiri ambazo huzificha attachments. Mmoja wa waajiri alitupa email mbadala ya Gmail, ambayo tulipoitumia alianza kupokea email zenye attachments vizuri bila matatizo. Waajiri wengine wawili hawakutupa email mbadala, hivyo ilitulazimu kuzifuta kazi zao kutoka kwenye site yetu.
Tunafanya kazi kubwa sana kuwaletea nafasi nyingi za kazi kila siku. Kama umekuwa unatuma maombi mengi ya kazi bila kuitwa kwenye mahojiano, kuna uwezekano mkubwa sana kuwa hauna vigezo vinavyohitajika kwa ajili ya hiyo nafasi au kuna watu wengine wengi waliotuma maombi ambao wana vigezo zaidi yako. Waajiri wengine huweka hili wazi kabisa, kuwa watawataarifu wale tu watakaokuwa ‘short-listed'. Lazima tuelewe kuwa kuna watu wengi sana wanaotafuta ajira kuliko nafasi za kazi zilizopo nchini Tanzania, hivyo kuna ushindani mkubwa sana katika kutafuta kazi. Wale wote ambao wanajua kuji-‘promote' vizuri na wanaotuma maombi kwa nafasi zile tu ambazo wana vigezo nazo, wana nafasi kubwa sana ya kupata kazi kuliko wale wasioweka jitihada katika barua za maombi na kufuata maelekezo ya mwajiri. Mtu mwenye vigezo na anayeweza kujieleza vizuri ndiye mwenye nafasi nzuri ya kuitwa kwenye mahojiano na kupata kazi.
Kama jitihada zako za kutafuta kazi hazijakusaidia kupata nafasi ya mahojiani, sisi
tunapendekeza usome mwongozo ambao tumeuandaa ili kukusaidia kukuongezea mafanikio katika kupata kazi >
ZoomTanzania | Job Seekers Guide. Ukisoma mwongozo huu kwa makini na kuzingatia mafundisho yake, utajiongezea nafasi ya kupata kazi nzuri.