Inatetea serikali ya mamaduro!heading yako ipo kuvuruga vichwa vya msomaji,maudhui yanaseam hivi heading inaleta tafrani unamchosha msomaji,
kwa kifupi hii bodi ya waandishi wa habari ni kama haipo siisiki ikitetea sana waandishi wa habari na stahiki zao,tasnia ya habari inapoteza mvuto
Nchi ya ajabu sanaMuda wote wanataka kusifiwa tu.
Bila CCM na amani nchini wewe usingezaliwa, mimba ya wewe isingepatikana. Iheshimu CCM, usifuate mkumboWote maCCM hai watajuana wenyewe
Bila hii bodi akina Zembela, Mpoki, Maulidi, nk wangeendelea kutamba kwenye habari bila cheti.Hii bodi ukiwa na cheti chake wanaweza kukutaza kulia msibani bila kibali chao
Wanasema alikuwa bar . Kwani mtu alitoka bar ndo hapaswi kutoa maoni yake juu ya jambo flani?Ashukuru kama hawajamuua
Pumbavu sijazaliwa TZBila CCM na amani nchini wewe usingezaliwa, mimba ya wewe isingepatikana. Iheshimu CCM, usifuate mkumbo
Wanajifanya yameisha watakuwa wanamlia timing kama yule dogo mchoraji.Ashukuru kama hawajamuua
bodi ya ithibati isiyokua na ithibatiJAB YAMPA ΟΝΥΟ ΚALI MWANDISHI KWA KUKIUKA MAADILI
Dar es Salaam, 23 Januari, 2026
Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), kwa mujibu wa mamlaka iliyopewa chini ya Sheria ya Huduma za Habari, Sura ya 229 na kanuni zake, imempa ONYO KALI Mwandishi wa Habari, Bw. Kelvin Justine Raphael, mwenye ithibati halali, maarufu kwa jina la ZUNGU (Matejoo) kufuatia kukiuka maadili ya taaluma ya uandishi wa habari katika maudhui aliyoyachapisha kuhusu tukio la uchelewaji wa ndege ya ATCL lililotokea tarehe 21 Februari, 2026.
Baada ya kumwita na kumpa fursa ya kusikilizwa kwa mujibu wa taratibu, Bodi imejiridhisha pasipo shaka kuwa mwandishi huyo alitoa kauli zenye matusi, kejeli na lugha isiyo ya staha na isiyozingatia mizania kinyume na misingi na maadili ya taaluma ya habari. Kauli hizo si tu zimekiuka misingi ya maadili ya uandishi wa habari, pia zimeathiri taswira ya taaluma ya habari na kuondoa heshima inayopaswa kuzingatiwa katika utoaji wa taarifa kwa umma.
Mwandishi husika amekiri na ameomba radhi kwa makosa hayo. Hata hivyo, Bodi imemtaka kuondoa mara moja maudhui hayo katika majukwaa yote aliyoyachapisha, kuacha mara moja tabia hiyo, na kurejea katika misingi ya maadili, weledi na uwajibikaji wa taaluma yake.
Aidha, Bodi inamwonya kuwa endapo atarudia au kuendelea na vitendo vya aina hiyo, haitasita kuchukua hatua kali zaidi za kinidhamu, ikiwa ni pamoja na kusimamisha au kufuta ithibati yake kwa mujibu wa Kifungu cha 14(b) cha Sheria ya Huduma za Habari, Sura ya 229 (Toleo la 2023).
Bodi inawakumbusha waandishi wote wa habari kuwa uhuru wa kutoa maoni na kujieleza hauondoi wajibu wa kuzingatia maadili ya taaluma. Taaluma ya habari ni nguzo muhimu ya jamii inayopaswa kuendeshwa kwa kuzingatia weledi, ukweli, uwiano na matumizi ya lugha yenye staha. Matumizi ya matusi, kejeli na lugha isiyofaa si tu yanadhoofisha uaminifu wa mwandishi binafsi, bali pia yanaharibu hadhi na heshima ya taaluma ya habari nchini.
IMETOLEWA NA:-
Patrick Kipangula
Kaimu Mkurugenzi Mkuu
Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB)
Kwani hiyo ndege kama kweli ilichelewa tatizo la Zungu ni nini kama sio uonevu?JAB YAMPA ΟΝΥΟ ΚALI MWANDISHI KWA KUKIUKA MAADILI