ZUWENA (Chaguo la wazazi)
SEHEMU YA: 01
MTUNZI: KHADIJA MWALAMI
WHATSAPP: 0676604830
KAWAIDA: 0783642467
ANZA NAYO........
SIMULIZI HII NI SH.1000 tu NICHEKI WHATSAPP KAMA UTAITAJI 0676604830β¦.
Katikati ya jiji la dar es salaam, kwa kawaida watu uliita jiji la biashara, na kweli pamechangamka bishara kila kona hadi kwenye vibaraza vya nyumba za watu.
Ikiwa ni mitaa ya kariakoo, anaonekana kijana mmoja ambaye anaonekana kuwa mpambanaji sana, anapiga debe uku na uku, sio sebe kwaajili ya abiria hapana.
Kijana huyo alikuwa akipiga debe ili wateja waingie dukani na kununua viatu.
"Weeh CRAY wenzio wanakula uko umeambiwa uingie ndani ukale kabla awajamaliza " ilizungumza mwanadada ambaye mavazi yake yalimtambulisha kuwa yeye ni muuza chakula pale kariakoo.
Kijana huyo aliingia ndani ya duka ilo na kukuta wenzie wakimalizia kupiga msosi, pasi na kunawa akainama ili aweze kula lakini alishtuka baada ya kupigwa bao moja la kuchwa.
"Unakulaje pasi na kunawa mwanangu unataka kutuwekea uchafu wako sio ? " alizungumza kijana ambaye alimpiga cray.
Cray alionekana kuwa zaifu kabisa hakujibu kitu, zaidi aligeukia kwenye sahani iliyokuwa na chakula na kukuta chakula kimeisha na kila mtu aliinuka na kupanguss mikono yake.
Cray aliishia kusikitika tu, maana chakula chenyewe ndo iko iko na wamekula pasi na kumuita.
Kijana Cray akatoka nje na kwenda kuendelea kupiga debe pale nje maana hakukuwa na kitu kingine cha kufanya.
Majila ya saa 1 jioni, duka lilifungwa na Tajiri akawalipa wapiga debe wake malipo ya kila siku kisha kila mtu akaondoka.
Cray aliingia mtaani kwao ambapo alikuwa akikaa kigogo, mitaa ya ndani ndani kabisa uko uswazi, vichochoro kama vyote yaani.
Cray alionekana kuwa mwenyeji kila alikopita alisalimiwa na kuchekewa hadi na watoto, akaingia kwa mama ntilie na kupata chakula kisha akaelekea magetoni pake ambapo alikuwa na godoro tu kuu kuu alilolitandika chini.
Chumba cha Cray kilipambwa na nguo zake alizotundika ukutani kwa misumali ikiwa ni njia moja wapo ya kitunza nguo zake.
Kijana huyo kitokana na uchovu wa siku nzima akajitupia kitandani pasi na kuoga akalala.
SONGA NAYO........
Niite Cray mtoto wa kwanza kabisa kwenye familia ya Mr and Mrs makato, nimekulia kijijini uko umakondeni Mtwara.
Baada ya maisha ya kijijini kuwa magumu Sana na harakati moja mbili tatu kubuma pale kijijini, nilifunga safari ya siri na kuja jijini dar es salaam.
Lengo la kuja dar es salaam ni kuja kutafuta maisha na kurudi nyumbani nikiwa na pesa ndefu nikiamini kuwa nikifika dar maisha yatakuwa marahisi na nitatoboa kwa muda mfupi.
Hali ikawa tofauti baada ya kuja Dar es salaam na kukuta life imekuwa ngumu sana, nilianza kulala barabarani, na kupigwa na jua mchana kutwa.
Niliogopa ata kuwasiliana na wazazi wangu na kuwaambia kuwa niko dar es salaam, hivyo nilikaa kimya uku nikiaidi kuwa siku nitakayopata pesa nitawasiliana nao na kuwafanya wajivunie mimi.
Baada ya maangaiko ya hapa na pale nilipata kazi ya kupiga debe kwenye duka la viatu ambapo kila siku nalipwa shilingi elfu 10 yaani kuanzia asubuhi mpaka jioni.
Boss wetu amekuwa mtu wa kutununulia chakula cha pamoja akidai kuwa kama mtu akiwa ashibi atajinunulia mwenyewe.
Niliweza kusave pesa na kulipa kodi ya miezi sita ambapo ni 25000 kwa mwezi mmoja maana mitaa yenyewe ni ya uswazi sana, yaani unaishi uku unaomba dua kwamba mvua isinyeshe π.
Maisha yangu yalikuwa ya mawazo sana nilitamani sana kuipigia familia yangu na kuwajulia hali lakini niliogopa kutokana na hali ya maisha ilivyo duni kwa upande wangu na wao na kwa muda huo waliitaji sana msaada wangu.
Miezi ilikatika hatimaye nikamaliza mwaka mzima pasi na kuwasiliana na wazazi wangu, na kipindi iko nilishaanza mahusiano na msichana fulani hivi mcharuko hatari.
Yaani mpenzi wangu maua hakuna kigoma au kigodoro kinachompita pale mtaani, yaani mimi ilikuwa ni mwendo wa kudaiwa pesa za sale tu, yaani vijora.
Kiukweli maua alijua kunichanganya, nilijikuta na furaha ambayo sio ya kawaida, nilihisi amani sana kuwa naye, na nikaanza kusahau kama nina ndugu na wazazi ambao naitaji kuwasiliana nao na kuwasaidia.
Siku hiyo nilikaa ndani nikiwa na mawazo sana baada ya kugombana na maua, nilijaribu kumpigia simu lakini hakupokea, sms pia hakujibu nilifunga safari na kwenda nyumbani kwao lakini familia nzima ilinifukuza kama mbwa nilijisikia vibaya sana kijana wenu π₯Ή.
Nilirudi nyumbani umoja ambao nimeuona kwa kina maua na wazazi wake ulinifanya nikumbuke familia yangu, nikavuta kidaftaro changu kilichokuwa na namba za watu wa nyumbani na kumpigia baba.
Simu ya baba iliita zaidi ya mara mbili, lakini haikupokelewa, na baada ya kukata tamaa, niliona simu yangu ikiita nilipoangalia ni baba ambaye nilipopokea tu simu ikakata nikajua alikuwa akibipu.
Haraka nikampigia baba ambaye na yeye alipokea muda huo huo.
"Hallo " niliweza kusikia sauti ya baba yangu ambayo sikuisikia takribani mwaka mzima π₯Ή.
Nilijikuta nikitetemeka cray Mimi, niliwaza baba atanipokeaje baada ya kuondoka nyumbani na kuwasusa kwa kuda mrefu.
"Hallo baba shikamoo " nilijikaza na kumsalimia.
Nyie damu nzito kuliko maji, niliposema tu shikamoo baba, niliweza kusikai sauti ya furaha ya baba akitaja jina langu kwa sauti ya juu.
"Ni mimi baba " nilizungumza kwa upole.
"Cray mwanangu tumekutafuta sana upo wapi ??" Baba aliniuliza.
Weeeh mama yangu ni mwanamke mkali sana, alivyosikia baba anaongea na mimi alimsogelea baba na kumpokonya simu kisha akaanza kunifokea.
"Mwana huna haya wewe, yaani unaondoka na kuacha familia kama umejizaa mwenyewe si ndio ? Ulitakq tufe kwa mawazo ? Na hatufi kabisa hatufi " maneno ya mama yalikuwa makali sana aiseeh nikijikuta nikiogopa.
"Mama cray, zungumza na mtoto vizuri haujui kama yuko saaa au laah hatujui ata yuko wapi ".
"Kokote alipo mimi sijali, na kama anataka nimsamehe kama mtoto wangu lazima aje nyumbani kuomba radhi kwangu la sivyo sitakuwa na radhi nae, mtoto kama sijamzaa mimi, cray unanisikia nakuomba uje nyumbani haraka iwezekanavyo la sivyo naomba usahau kwamba una familia "
Daaah mama alifoka sana hakunipa ata nafasi ya kuzungumza na alivyoona amemaliza maongezi yake alichofanya ni kukata simu.
DAAH EBU NIAMBIENI NIFANYE NINI CRAY MIMI π₯Ή
ITAENDELEA....
ZUWENA (Chaguo la wazazi)
SEHEMU YA: 02
MTUNZI: KHADIJA MWALAMI
WHATSAPP: 0676604830
KAWAIDA: 0783642467
SONGA NAYO.......
Baada ya maneno ya mama kuwa makali na kukata simu yangu, nilibaki kuwa mtu mwenye mawazo sana, kuna muda niliwaza ata kwanini nimewapigia.
Usiku wangu ulikuwa mzito sana niliwaza sana maneno makali ya mama, ata ajui naishije uku, ajui kijana wake shida ninazopitia.
Nilikaa Macho usiku kucha, niliamka asubuhi nikakoga na kudandia daladala ambayo ilinifikisha mpaka msimbazi.
Nilifika dukani na kuanza na shughuli yangu ya kupiga debe, siku hiyo boss sijui alipatwa na nini jamani, alikuja na kutuambia kuwa kila mtu atakuwa anajitegemea chakula asubuhi mchana na jioni.
Daaah π nikiwaza sana, sasa elfu 10 na nitakuwa nakula nini na kuweka akiba kweli, maana ule asubuhi mchana jioni, hapo bado nauli na ujanywa maji ukiwa kazini.
Maana kazi zetu za kupiga kelele hizi maji ni muhimu sana.
Nilijikuta tu nikikosa furaha niliwaza maneno ya mama pia nilichoka zaidi, kichwa kikawa kinaniuma kabisa baada ya kuwaza na kuwazua kwa muda mrefu.
Niliona kabisa kichwa kinavyoniuma na kazi ya kupiga kelele sitaweza, nilichofanya ni kuomba ruhusa kwa boss ili niweze kwenda kupumzika.
Boss aliniruhusu lakini ndo hakunipa ata elfu mbili π₯Ή nilichofanya ni kwenda kudandia gari na kurudi mtaani kwangu.
Nilipita nyumbani kwa kina maua ili niweze kuzungumza nae na tumalize ugomvi wetu lakini ilikuwa kasheshe, tena ni kama nikijiloga kwenda mchana nilikuta akiwa na shoga zake walahi walijua kunisuuza mwanaume mimi.
Nikipewa kila aina ya maneno, nilichambwa na kuoshwa vya kutosha sijui mnaelewa πππΏ.
Nikajaziwa na watu, yaani mitaa ya uswazi bhana kitu kidogo tu watu shazi, nilijua kuumbuka mwana wa mwenzenu π.
Mwenyewe polepole, nikakusanya ndala zangu na kuzishika mkononi na kukimbia maana hakukuwa na nguvu ya kutembea pale, yaani nilizomewa hadi na watoto wadogo.
Basi nilifika nyumbani kwangu na kujitupia kwenye godoro langu nahema kama mbwa aliyedokoa nyama za mama ntilie.
Baada ya muda nilipitiwa na usingizi nilikuja kustuka saa 11 jioni nilichoka mno ukizingatia njaa pia ilikuwa imeshika nafasi yake.
Niliinuka na kuingia mtaani, nikanunua Unga na dagaa mchele na kimfuko changu cha mkaa.
Nilifika nyumbani nikakoleza moto mtoto wa kiume nikatoa kitu pale, yaani hakuna kumbwela, saa 1 usiku ugali ulikuwa umeshakwiva na nilikaa chini na kupiga kitu.
Baada ya kushiba sasa ndo nikamkumbuka mpenzi wangu maua πππΏ ila njaa mwana alamu, nilichukua simu na kumpigia maua, alipokea na kunipolomoshea matusi uku akiniambia kuwa anitaki tena kwani amepata mwanaume mwenye pesa zake.
Nilikuwa mnyonge sana kijana wenu, kwani maua ndio mwanamke wa kwanza kwa upande wangu na ndio ameniingiza kwenye dunia ya mapenzi
*********
Mwezi mzima uliisha, mambo hayakuwa vizuri kwa upande wangu, nikasema hapa lazima nirudi nyumbani kwani inaweza ikawa ni hasira ya mama ndo inafanya kazi kwa kasi hivyo.
Basi kwakuwa nilikuwa na viakiva vyangu, nilichukua na kufanya nauli na pesa nyingine nilijaribu kuwanunulia ata vizawadu kidogo maana sio unaenda nyumbani mikono mitupu.
Safari ilikuwa ndefu sana lakini kwa uwezo wa Mungu nilifika salama salimini, baba alifurahi sana kuniona.
Mama pia yaani alifurahi mno alinikumbatia uku akilia, yaani hakuwa na hasira kama siku ya kwanza.
Kiu ya mama yangu ilikuwa ni kuniona mimi kijana wake na alivyoniona hasira zote zilimuisha kwakweli nilijisikia amani kuonana na familia yangu kwa mara nyingine.
Niliwapatia zawadi zao, kwanza ndugu zangu wote wakaamini kuwa kweli kaka yao ni mpambanaji ukiangalia nilirudi na mavazi mapya.
πππΏ ila watu wa mkoani bwana sijui wakisikia dar wanaonaje, kijiji kizima kilijua kama nimerudi, mama alikuwa anawaambia mashoga zake wote.
Ikiwa ni majila ya usiku nikiwa home nimejaa nje, nilimuona mama akija na msichana fulani hivi mzuri mno yaani.
Msichana huyo, hakuwa mgeni kwangu na nilikuwa nikipenda sana kumuangaliaga enzi hizo, na ndo nilikuw anajuaga dunia nzima yeye ndo mzuri.
Ila nilipofika dar na kukutana na wapaka make up ndo nilipoona kuwa msichana wa kijijini kwetu ni wa kawaida mno.
"Cray umemuona zuwena ??" Mama aliniuliza uku akicheka cheka.
Nilimuangalia mama nikatabasamu na kujibu.
"Nimemuona mama "
Zuwena mwenyewe alikuwa ni msichana mpole sana na ana aibu mno, muda wote alikuwa ameshikilia sketi yake akiizungusha kana kwamba alikuwa akikung'uta maji.
Basi nilisalimiana na zuwena pale kisha akaondoka, na kwakuwa ilikuwa ni usiku mama akaniomba nimsindikize, nilibaki nikijiuliza sasa nyumbani alikuja kufanya nini ?? Yaani baada ya kusalimiana na mimi tu na safari ya kurudi kwao imefika πππΏ.
Basi mwaya kama unavyojua vijijini ni vichaka tu, alionekaka kuwa muoga, nilichofanya ni kumshika mkono ili kumjuza kuwa tupo pamoja.
Nilimfikisha mpaka nyumbani kwao, niliwasalimia wazazi wake na kuwaaga ili kurudi nyumbani.
Yaani na lile giza na vile vichaka, nilitamani kuvua viatua na kushika mkononi, ili nikimbie vizuri.
Yaani nikikimbia kana kwamba nilikuwa nikifukuzwa π niwaambie tu wanawake mnavyokujaga magetoni halafu tunawasindikiza usiku uwaga tunarudi home kwa kukimbia na muda mwingine uwa tunabeba na Mawe kwaajili ya kujiamiπππΏ.
Nilifika nyumbani nikiwa nahema sana natokwa na jasho, tu, kwakuwa kwetu kulikuwa na kisima niliteka maji na kwenda kukoga.
Mwisho familia nzima tulikutana ndani na kupata msosi, sisi familia zetu ni zile za kuweka sinia kubwa na kukaa duara, kwanza kwa upande wangu uwa ndo naona raha sana.
Baada ya kumaliza chakula, wote wakatawanyika, ila baba akaniomba kwa kusema kuwa anamaongezi na mimi.
"Cray kijana wangu, kwanza nikupongeze, umekuwa kijana wangu na umekuwa mwelevu sana, na ninakuombea Mungu akufungulie milango yote ya mafanikio " alizungumza baba.
"Amina baba "
"Sasa, ukiachana na ukuaji na utafutaji, na kila kitu, mimi kama baba yako naona umri wa kuoa umefika lazima upate mwenzio wa upande wa kushoto "
"Daah mzee Muda bado, halafu mimi sina plan ya kukaa hapa kijijini narudi tena mjini " nilianza kujielezea.
"Na hakuna mtu atakuzuia wewe kuondoka, na utaondoka na mke wako zuwena "
Nyieeeh ππΏπ kwahiyo kumsindikiza siku moja tu tayali amekuwa mke wangu ? π aaah baba bhana.
"Baba ebu subili, mke wangu zuwena ? Nimeoa lini ??"
"Tumekuolea, na alikuwa akikusubili miezi yote hiyo ni binti mzuri na mwelevu utaondoka nae akakusaidie anajua kulima na kutunza mifugo "
"Baba alitekuwambia dar tunalima ni nani ??, halafu mimi tayali nina mwanamke wangu"
Weeh kitendo cha kusema hivyo ni kama nilijiloga uwiiiih ππΏ ata sijui mama alifika saa ngapi nilishtukia tu nikipigwa ndala ya mgongo.
ILA WAMAMA WA KIAFRIKA NA SIRAHA ZAO ZA NDALA ππ
ITAENDELEA
ZUWENA (Chaguo la wazazi)
SEHEMU YA: 03
MTUNZI: KHADIJA MWALAMI
WHATSAPP: 0676604830
KAWAIDA: 0783642467
SONGA NAYO.......
Nilishtuka sana, na kushuka mgongo wangu maana mama alitumia nguvu zote kunitandika na ile ndala aliyoishika kwenye mkono wake.
Niliinuka na kuingia chumbani kwangu, maana pale maelewank yalishaisha kabisa, maana mama angu akiwaga na hasira kuongea nae na kuelewana ni ndoto.
"Mpuuzi sana wewe, yaani uko sasilamu, ndo kumekufanya uwe na jeuri kiasi iko si ndio ? Sasa nakuambiaje, hakuna kurudi uko, bila izini yangu hakuna sehemu unaenda we paka mmoja tu "
"Eeeh mama cray usiku huu kelele zote za nini kuwapigia majilani washindwe kilala ? Halafu unaongea kwa sauti hivyo unataka kumpa faida nani ??" Baba na yeye kama mwanaume akapaza sauti.
"Eeeh haya endelea kunifokea sasa, mimi si sina kauli kwa kijana wangu, haya wewe si baba yake, mimi sio mama yake haya nifokee, uwiiiiih Mungu nimekosa nini mimi "
Mama yangu ni mtu wa drama sana yaani vitu kidogo tu, anachukulia kwa ukubwa, yaani hapo ameanza kujiliza ili aonekane ameonewa.
"Tatizo lako ndo ili hautaki kuambiwa ukweli, na ukiambiwa unaanza kutengeneza scene nyingine, kwa upande wangu niseme kuwa sina la ziada mpaka kufika hapa usiku mwema "
Daaah nilikaa ndani na kusikiliza kelele za wazazi wangu, na sababu kubwa ya wao kubishana kama hivyo ni mimi.
Kiukweli, sikuwa tayali kuwa na mahusiano na zuwena, lakini pia ukizingatia mimi nina mchumba wangu mwingine nimemuacha mjini uko.
Sawa mimi na mpenzi wangu maua hatuna maelewano, lakini haiwezi kuwa sababu ya mimi kumkubali zuwena, miaka yote zuwena nimemuona kama dada yangu tu na sio mwanamke ambaye ni wa ndoto zangu.
Usiku wangu ukawa mzito kwa mara nyingine, yaani kuna akili ilikuwa inaniambia toroka tu, na uondoke kama mwanzo.
Halafu akili nyingine inaniambia, ukuondoka na kuwaacha wazazi na kinyongo basi matatizo yatakuwa halali yako.
Kwakweli nilikosa jibu kabisa.
Asubuhi niliamka na kwenda nje kufagia uwanja, kwani mbele ya nyumba yetu kulikuwa na kiwanja kikubwa sana, ambacho hakikuwa na nyasi, na kilikuwa kinachafuka kwaajili ya mtu mkubwa wa mkungu uliopo hapo nyumbani.
Nilianza kusafisha uwanja, polepole, mwenyewe, uku nikiendelea kujiuliza maswali mengi Sana juu ya zuwena na mama.
Najua baba awezi kunifosi kumuoa zuwena lakini mama sasa eeeh, mama yangu ni mtambo akiwa na jambo lake anahakikisha linakamilika.
Nikiwa bize bafagia, nikishangaa sana kumuona zuwena akija na mtungi wa maji amebeba kichwani, na nyuma ya zuwena alikuwako mama ambaye alikuwa akija polepole.
"Kwahiyo hauta mtua binti wa watu hayo maji kuchwani mwake ??"
Eeeh mama yangu sasa, akaanza na lawama, zake. Nikatupa ufagio na kumsogelea zuwena, hapo nilinsaidia kushusha ule mtungi wa maji na kuweka chini.
"Asante " alizungumza zuwena baada ya mimi kumtua maji.
"Usijali" nilijibu na kuingiza mtungi wa maji ndani.
Nilitoka nje na kushika ufagio wangu na kuendelea kufagia, muda huo, mama aliingia jikoni, jiko letu wenyewe la nyasi, mama akatoka akiwa amebeba ungo ukiwa na miogo na kisu.
Niliacha na kufagia kwanza nikabaki nikimuangalia mama nilitaka kujua huyu bi mkubwa amepanga kufanya nini.
Mama akamkabizi ule ungo zuwena na kuingia ndani akatoka na mkeka wakatandika chini ya mti, hapo zuwena akaanza kumenya ile miogo.
"Kwahiyo asubuhi yote hii ameshindwa kufanya kazi nyumbani kwao amekuja kufanya nyumbani kwetu ? " nilijikuliza kimoyomoyo tu.
"Unataka kumaliza kufagia saa 8 mchana au ??" Mama alinifokea baada ya kiona nimeganda tu.
Basi haraka nikamaliza kufagia na kuingia chumbani kwangu, kwakuwa na mimi nilikuwa nimejifanya mtu aa mjini, nilienda na sabuni zangu zile za kunukia za bukubuku πππΏ.
Nilichukua sabuni na Taulo langu ambali nililitupia tu shingoni na kutoka nje.
"Mama naenda kuoga mtoni " nilimuaga mama.
Mama aliinua shingo yake akanitazama weeh, mwisho akaachia sonyo moja matata, kisha akamuangalia zuwena na kumwambia.
"Msindikize mwenzio mtoni "
Eeeeh nilibaki nikiwa nimetoa macho tu, π³ yaani naenda kuoga halafu niende na zuwena anataka akanichungulie au ni kitu gani.
"Mama jamani naendaje kuoga mtoni na mtoto wa kike "
"Sio mtoto wa kike tu huyu ni mke wako sawa, lakini pia sikuamini unaweza ukatoloka"
Daaah zuwena alikuwa akimuigopa sana mama alichofanya ni kuinuka na kuongozana na mimi.
Nilikuwa nikitembea kwa kasi sana, mimi mbele zuwena nyuma sikuwa najali kuhusu yeye ata kidogo, kuna muda alikuwa amekanyaga mwiba ambao ulitoboa ndala yake na kumchoma lakini sikujali.
"Aaah cray naomba nisaidie kutoa huu mwiba " zuwena aliniomba.
"Kulikuwa na haja gani ya wewe kuja uku ? Si ungebaki nyumbani au ??"
"Nawezaje kupinga kauli ya mama mkwe ??" Zuwena akaniuliza.
Hapo nikajua huyu msichana nae kumbe ni kiazi kabisa, yaani ameanza kumuita mama yangu mkwe kabisa π ila wasichana bhana ata awajionei huruma.
"Ilo Neno mkwe futa sawa ? Zuwena nikuambie ukweli, hautakuja kuwa mke wangu na wala sitakuja kukuoa"
"Niwe mke wako mara ngapi ?" Zuwena aliniuliza.
"Mara ngapi vipi nawe, MI sitakiwa kuwa mnafiki kwako zuwena, sikupendi, sijutaki sikuitaji "
"Kama ni hivyo, itakupasa kuniandikia taraka na kuachana na mimi kwa utaratibu maalumu kabisa"
"πππΏ ata uchumba bado unataka taraka, we kweli pimbi"
"Ukweli ni kwamba mimi na wewe ni mke na mume, na wazazi wako ndio walikuolea, ubaki umepitishwa na mahali wazazi wangu wamepokea, mwezi wa nne sasa naishi pale kwenu kama mke halali wa cray "
"Nini ??"
"Umenisikia, kutokunikuta haimaanishi kuwa naishi kwetu, nilienda kwetu kwaajili ya kumuuguza mama yangu na sasa hivi anaendelea vizuri nimerudi kwenye ndoa yangu ".
Kwanza ata safari ya kwenda mtoni ilikufa kabisa, nikafunga safari na kurudi nyumbani chapu, hapo hasira kama zote.
"Mama,mama , mama " nilifika nyumbani na kuanza kumuitilia mama kwa hasira kwani sikumkuta pale nje.
"Nini nawe mikelele " alifoka mama baada ya kutoka nje.
"Mama anachoniambie zuwena ni kweli ? Yaani ninyi mmeshaniolea zuwena ??"
"Sasa cha ajabu ni kipi hapo ?"
Daaah mama yaani aoni kama kuna shida na anaona kila kitu powa tu.
"Mama mnanikosea sana, yaani mnanioleaje mwanamke mkiwa amjui kama nilikuwa hai au nimekufa ? Eeeh hakuna kitu mmeongea Na kila kitu mnajiamulia " nilimfokea mama kwa sauti ya juu sana
"Ukimaliza kupaza sauti kwa mama yako, njoo unipazie na mimi ambaye nimelipa pesa ya mahali "
Weeh ilikuwa sauti nzito kabisa ya baba, nilibaki nikimtolea macho tu.
"Lakini mnanikosea sana " nililalamika lakini kwa sauti ya chini sana, nilikimbilia ndani na kujifungia.