abiria

Abiria (kutoka neno la Kiarabu عبر ˁabara kwa maana ya kuabiri, kuvuka eneo la maji) ni watu wanaosafiri kwa kupanda meli, ndege, gari, basi, pikipiki au treni.

Abiria hutumia vyombo hivyo vya usafiri kama njia ni mbali, au kama hawana usafiri wa binafsi au kama wanapendelea matumizi ya usafiri wa umma kuliko usafiri wao binafsi.

Kwa kawaida wakipanda wanalipia kiasi fulani kama nauli ili mwenye chombo hicho aweze kuwalipa dereva na wahudumu wengine pamoja na gharama za chombo chenyewe na matumizi yake.
  1. Mjanja M1

    Korogwe: Bodaboda wadaiwa kuchoma basi la Saibaba baada ya mwenzao kugongwa

    Basi la Kampuni ya Sai Baba linalofanya Safari kutoka Dar es Salaam kuelekea Mkoani Arusha limeteketezwa kwa Moto mara baada ya kusababisha Ajali kwa kumgonga Dereva wa Bodaboda na kudaiwa kusababisha kifo kwa dereva huyo wa Bodaboda katika eneo la Msambiazi wilayani Korogwe mkoani Tanga leo...
  2. I am Groot

    Rais kutumia ndege ya abiria badala ya ndege yake binafsi, nani mshauri wake?

    Jamani ndege kama hii BOEING 737-9 max ni ndege ya gharama sana achana na ununuzi wake tu bali hata maintenance pia. Inasikitisha kuona Rais anatumia ndege hii yenye gharama kiasi hiki huku ndege ya Rais ikiwepo bado. Sitashangaa ikipata hitilafu tukaitelekeza mahali kwa sababu matumizi yake...
  3. Yoyo Zhou

    Ndege kubwa ya abiria ya C919 yashiriki kwenye Maonesho ya Ndege ya Singapore

    Ndege kubwa ya abiria ya C919 ya China hivi karibuni iliwasili nchini Singapore ili kushiriki kwenye Maonyesho ya Ndege ya Singapore ya mwaka 2024 yanayofanyika siku hizi. Hii ni mara ya kwanza kwa ndege kubwa aina ya C919 ya COMAC inayozalishwa nchini kuonekana nje ya nchi. Hali hii inaonesha...
  4. Zanzibar-ASP

    KERO Utingo wa Basi la kampuni ya Dolphin Express (njia ya Dodoma-Arusha/Moshi) ndio kinara wa kuibia abiria

    Kama ulikuwa hujui hilo basi sasa anza kuchukua tahadhari mapema. Ama usipande kabisa hilo basi au ukipanda huku ukikaa kwa tahadhari kubwa sana, maana utingo wa basi ndio mastermind. Kampuni ya mabasi ya Dolphin Express kwa sasa huenda ndio inaongoza kuwa na makondakta (utingo) wezi wa mali za...
  5. BigTall

    Abiria wanapanga foleni lakini bado changamoto ya Mwendokasi ni kubwa

    Mbali na kuwa na utaratibu wa kupanga foleni lakini bado usafiri wa Mwendokasi Kituo cha Mbezi Luis Dar es Salaam bado ni changamoto sana, sijui nini kifanyike kwa kweli? Nimepita nikaona watu wanavyopambana na kugombania kuingia kwenye usafiri hadi huruma.
  6. Mjanja M1

    Bodaboda jela miaka 30 kwa kumbaka abiria wake mkoani Kigoma

    Mahakama ya Hakimu Mkazi Uvinza imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela dereva wa bodaboda, Ruben Gerishon (24) mkazi wa Kijiji cha Mlela wilayani humo mkoani Kigoma baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka abiria wake. Sambamba na hukumu hiyo, mahakama imetaifisha pikipiki iliyokuwa ikitumiwa na...
  7. B

    Serikali piga marufuku mrundikano wa abiria kwenye Daladala

    Yaani kuishi nchi hii ya Tanzania imekuwa nongwa sana, kila eneo wafanyabishara wanajiamlia kufanya yao. Waendesha daladala wanapakia abilia hadi mlangoni, watu wanasimamiahwa na kupangwa kama magunia ya mikaa. Kwani serikali hatuwezi kufanya hata hili la usafiri kwa kuzingatia level seat nchi...
  8. Stephano Mgendanyi

    Serikali Iko Mbioni Kujenga Uwanja wa Ndege Zenye Uwezo wa Kubeba Abiria 50 Mkoani Singida

    Katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni jijini Dodoma, Mhe. Martha Nehemia Gwau aliuliza swali lililojibiwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. David Kihenzile na kusema kuwa Serikali iko mbioni kujenga uwanja wa ndege wa daraja 2C Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, Mhe. Martha Nehemia...
  9. T

    Wizara ya afya Tunaomba mchunguze uwepo wa kunguni na mende wadogo kwenye mabasi ya abiria safari ndefu

    Serikali kupitia wizara ya afya Tunaomba mfanye ukaguzi kwenye mabasi ya usafirishaji wa abiria hasa safari ndefu jamani mabasi yana kunguni na mende wadogo wengi jambo lina hatarisha afya ya abiria. Siku zakaribuni nikiwa na abiria wenzangu tulishuhudia utitiri wa kunguni kwenye basi la...
  10. Ghost MVP

    Mabasi ya abiria ni machafu, Nacharo T 706 DVF wajirekebishe

    Nawasilisha hili kwa wasafiri wenzangu wa mara kwa mara na kwa wenye nafasi ya kufikisha taarifa hii kwa wahusika. Kuna kampuni ya usafirishaji abiria inaitwa Nacharo Royal Bus, ambao hufanya safari za Tanga Dar nk. Kuna hili bus lao moja usajili wake ni T 706 DVF ni chafu linanuka uvundo na...
  11. Kakondele

    Tunauza Magari Makubwa na madogo ya aina mbalimbali

    Basi lenye Terias injini ya scania 113 hoarse power 320 body limetengenezewa kenya linauzwa lipo katika hali nzuri na hivi sasa linatembea na injini yake haijawai kuguswa.bei yake ni rahisi ambayo hata watu wahali ya chini wanaweza kumudu kwa mawasiliano zaidi bei ni tzsh mil 50,000,000 sababu...
  12. Ghost MVP

    Mwanajeshi kumshambulia dereva wa daladala ikiwa na abiria ni kuhatarisha maisha ya abiria pia

    Kuna Mkasa umtokea ukimuonesha Mwanajeshi wa JWTZ akimshambulia Dereva wa daladala ya Tabata, Lakini Akiwa anafanya Tukio hili Dereva wa Daladala alikuwa hajaweka gari katika 'Parking' Hivyo ikawa inatembea, Hii ni hatari kwa maisha ya abiria walioko katika Daladala hiyo na Wale wanaotumia Kwa...
  13. JanguKamaJangu

    Abiria wa Treni ya TAZARA washushwa mpakani ili Treni Ipulizwe Dawa ya kuua vimelea vya Kipindupindu

    Abiria wa Treni ya TAZARA iliyotoka Zambia wameshushwa mpakani Tunduma ili Treni ipulizwe dawa ya kuua vimelea vya Ugonjwa wa Kipindupindu. Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Dr. Enock Mwambaraswa amesema hatua hiyo imekuja kutokana na taarifa za kuwepo kwa Ugonjwa wa Kipindupindu...
  14. uran

    Picha: Meli kubwa ya abiria, Norwegian Dawn imetia nanga Dar 16.01.2024

    Imekuja na Watalii zaidi ya 2,000. Mama anafungua Nchi. #VisitTanzania#
  15. A

    DOKEZO Sehemu ya kusubiria abiria Kivukoni joto ni kali na feni hazifanyi kazi

    Kuna tatizo tunaomba Serikali, Jamii na hasa mamlaka husika zifahamu ili hatua zichukuliwe, ni kuhusu kero ya joto kutokana na msongamano wa watu Kivukoni Jijini Dar es Salaam. Abiria tunaotumia vivuko tunapata shida sana wakati wa kusubiri Kivuko kwenye lounge kutokana na joto kali...
  16. JanguKamaJangu

    Somalia: Helikopta ya Umoja wa Mataifa (UN) yashikiliwa na Al-Shabab ikiwa na abiria

    Kundi la Al-Shabab limeikamata Helikopta ya Umoja wa Mataifa (UN) ikiwa na Watu Wanane wakati ilipotua kwa dharura katika eneo linaloshikiliwa na kundi hilo katikati mwa Somalia. Kituo cha Habari cha Somali National News Agency (SONNA) kimeeleza Ndege hiyo ilitua Mji wa Galmudug na mazungumzo...
  17. Nyafwili

    Madereva wa mikoani, tabia na utaratibu wa kupaki mabasi sehemu ya chakula chenye bei juu mnaumiza abiria wenye kipato kidogo

    Serikali yetu - mamlaka husika tunaomba mtusaidie sisi wanyonge na hii tabia ya madereva inayozidi kushamiri kila kukicha, hasa kwa wale ndugu zetu wanaosafiri mikoa ya mbali wanapata tabu sana kuhusu masuala ya chakula. • Dar - - Mwanza • Dar - - Mbeya • Dar - - Kigoma • Dar -- Arusha • Dar --...
  18. Ndagullachrles

    LATRA yaokoa jahazi abiria wa Rombo

    Kama mnavyojua ndugu zetu wachaga wanavyosifika kurudi makwao mwishoni mwa Mwaka au "kwenda kuhesabiwa"kama inavyojulikana na wengi,basi idadi ya mabasi ya kuwasafrisha huwa inazidi namba ya abiria. Kutokana na Hilo,Maofisa wa Mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa ardhini(LATRA)katika mkoa wa...
  19. MAWEED

    Hamis Chaurembo: Dereva mjinga aliyeuwa abiria kwa mwendokasi Kigoma

    Aliyekuwa Dereva na mmiliki wa gari ndogo, Hamis Chaurembo (27) maarufu kama SIMBA ambaye amefariki baada ya kupata ajali mbaya huko Kibondo Kigoma amezikwa jana. Ila kuna cha kujifunza hapa kutokana na maneno ya baadhi ya marafiki zake. "Baadhi ya A.K.A alizopambwa nazo ni pamoja na 'Mwendo...
  20. Roving Journalist

    Madereva wa mabasi ya abiria watakiwa kuacha matumizi ya vilevi kuepuka ajali

    Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani limefanya ukaguzi wa mabasi ya abiria katika Stendi Kuu ya Mabasi kabla ya kuanza safari na kuwataka madereva kuzingatia Sheria, Kanuni, Alama na Michoro ya Usalama Barabarani ili kuepuka ajali. Akizungumza Disemba 23, 2023...
Back
Top Bottom