Albert Chalamila, akiwa Mkuu wa Mkoa katika mikoa tofauti, alijipatia umaarufu kutokana na kauli zake tata na zingine ambazo mara nyingi ziliwaacha watu hoi. Akiwa katika Mkoa wa Mbeya, aliwahi kusikika akitoa agizo la kuchapa viboko wanafunzi walioteketeza mabweni, jambo lililozua mjadala...