Paukwa tena pakawa, mtaani taharuki
Bibi kanyoa kipara, na nywele tena hasuki
Chaajabu kina chawa, kichwani hawabanduki
Bibi kanyoa kipara, mtaani taharuki
Mtaani wauliza, hiki kipara chanini
Mana wengi chawaliza, madukani na saluni
Ma tena chaleta giza, biashara taabani
Bibi kanyoa kipara...