chadema

CHADEMA (Chama cha Demokrasia na Maendeleo)
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni chama cha kiasiasa nchini Tanzania ambacho kilianzishwa tarehe 28 Mei 1992 na mwanasiasa mkongwe Edwin Mtei, aliyewahi kuwa Waziri wa Fedha katika miaka 1997 hadi 1979.

Mwaka 2000 CHADEMA hakikuwa na mgombea wa Urais. Mwaka 2005 mgombea wa CHADEMA Freeman Mbowe alikuwa namba tatu kati ya wagombea kumi akapata asilimia 5.88 za kura.

Mwaka 2010 CHADEMA ilipata asilimia 27.1% na mgombea Urais wa chama Wilbroad Peter Slaa na kura 4,627,923 kwa 31.75%.

Hata hivyo CHADEMA imekataa matokeo mengi kutokana na mchakato mzima kuwa mikononi mwa Tume ya Uchaguzi isiyo huru.
  1. comte

    Aliyekuwa mgombea nafasi ya Uenyekiti BAVICHA: Lissu na Heche walitia doa kampeni za Uchaguzi wa BAVICHA

    Mgombea Uenyekiti BAVICHA Masoud Mambo akifunguka A to Z kilichotokea kwenye Uchaguzi BAVICHA baada ya wakubwa kuingilia kati. Source: East Africa Radio My take: Usafi wa Heche na Lissu uko mdomoni tu- ni wachafu kuliko uchafu wenyewe
  2. Erythrocyte

    Pre GE2025 Baraza Kuu la CHADEMA laidhinisha Wagombea wa Juu wa Uongozi wa Chama hicho, kwahiyo Kipute kiko pale pale

    Katika vikao vya Baraza Kuu vinavyoendelea leo hii, tayari mambo kadhaa yameanza kutolewa maamuzi. La kwanza ni hili la kuidhisha mtanange wa Wagombea wa Juu wa uongozi wa Chama hicho. Taarifa yao hii hapa Usiondoke JF kwa Taarifa za uhakika za Vikao hivi, Hii ni kwa sababu Mimi Mtumishi...
  3. Tlaatlaah

    Pre GE2025 Huenda vurugu na ghasia zikahamia kwa muda kwenye uchaguzi wa CHADEMA Taifa

    Joto la kisiasa linaloendelea kupanda kila uchwao miongoni mwa kambi hasimu za wagombea uenyekiti wa chadema taifa, huenda likaishia kuwasha moto wa ghasia na fujo kutokana na kujipiga kifua kwa kila kambi kwamba, ndiyo yenye haki na uhalali wa kushinda uchaguzi huo dhidi ya kambi nyingine...
  4. Robert Heriel Mtibeli

    Pre GE2025 Lissu ukishinda Uenyekiti CHADEMA Taifa pitisha Ubatizo wa utakaso kwa Wala Rushwa wote ndani ya chama...

    Mpo salama! Ni hakika Kesho Lisu anashinda. Ubatizo wa Utakaso "Baptism of purification" ndio Jambo pekee ambalo Lisu itampasa aanze nalo. Hakuna haja ya kugombana, kuvunja Chama. Mshindi amepatikana sasa ni Muda wa kuwekana Sawa. Wale wenye shutuma za Rushwa na waliofanya Rushwa wafanyiwe...
  5. P

    Pre GE2025 Lissu na Mbowe uso kwa uso kwenye kikao cha Baraza Kuu CHADEMA 2025

    Kikao cha Baraza Kuu la CHADEMA 2025 kinafanyika muda katika makao makuu ya chama yaliyopo Mikocheni, ambapo viongozi wakuu, Freeman Mbowe na Tundu Lissu, wakutana uso kwa uso. Huu ni mkutano muhimu unaojadili masuala mbalimbali yanayohusu mustakabali wa chama kuelekea kesho Januari 21 kwenye...
  6. Waufukweni

    Pre GE2025 Mnyika alivyowatambulisha wagombea CHADEMA Mkutano wa Baraza Kuu, ukumbi walipuka alipotajwa Lissu

    Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Januari 20, 2025 ulilipuka kwa shangwe kutoka kwa wajumbe wa mkutano wa Baraza Kuu la Chadema unaoendelea baada ya Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika, kuwatambulisha wagombea wa ngazi ya juu ya uongozi wa chama hicho. Mnyika...
  7. E

    Pre GE2025 Januari 21, 2025 nchi itazizima ni kishindo kufuatia Uchaguzi Mkuu CHADEMA

    Habari njema itawaamsha waliolala kwa kukosa MATUMAINI waliokata tamaa kujaa Furaha walioshindwa kutembea KURUKARUKA wasio ona KUONA walio na KIU kuuona mto walio na machozi KUFUTWA Kesho NYATI anafunguliwa zizini nyati anakwenda KUTUONGOZA kuchanja MSITU Hotuba ya KUSISIMUWA itapasuwa Mioyo...
  8. Doctor Mama Amon

    Mkutano Mkuu Chadema Kesho Kujibu Mapigo Dhidi ya CCM kwa Kusimka Lissu Mwenyekiti Taifa, Kumtangaza Mgombea Urais 2025 na Kumpatia Mgombea Mwenza?

    Mhe. Tundu Antipas Mughway Lissu, Mwenyekiti Mtarajiwa wa Chadema na Mgombea Urais Mtarajiwa Katika Uchaguzi wa 2025 Kutokana na mikutano mikuu ya Chadema na CCM inayofanyika kwa kufuatana ndani ya Januari 2025 sasa ni wazi kwamba busara kongwe za wanazuoni zitaanza kutimia. Wanazuoni wengi...
  9. Manyanza

    Pre GE2025 Hoja za Tundu Lissu Kuhusu Mwelekeo wa CHADEMA zinamtoa hatiani Zitto Kabwe

    Nimefanikiwa kuusoma unaoitwa Waraka wa Mabadiliko 2013 uliotayarishwa na Samson Mwigamba, aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Arusha, na kuhaririwa na Kitila Mkumbo, aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama, uliolenga kumuuza Zitto Kabwe, wakati huo akiwa Naibu Katibu Mkuu wa chama, kwa...
  10. S

    Pre GE2025 Hivi wanasiasa wa CHADEMA wakihamia CHAUMMA leo, sheria inawaruhusu kuwa wagombea kupitia CHAUMMA kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu?

    Habari wadau! Kama kumbukumbu zangu ziko sawa, sheria ya uchaguzi ilifanyiwa mabadiliko enzi za Mwendazake lengo ni kudhibiti watu kuhamia vyama vingine uchaguzi unapokaribia. Kwa kumbukumbu zangu, kuna mdau ambao mwanachama anatakiwa awe mwanachama wa chama husika Kama kigezo cha kuruhusiwa...
  11. Waufukweni

    Pre GE2025 Dosari na Rafu kwenye Uchaguzi Mkuu wa CHADEMA Taifa 2025

    Rushwa na vurugu zimeikumba CHADEMA katika uchaguzi wa Taifa 2025 uliofanyika Januari 13 na 16, ambapo mabaraza ya vijana (Bavicha), wazee (Bazecha), na wanawake (Bawacha) yalichagua viongozi wapya. Hata hivyo, baadhi ya wanachama walidaiwa kupokea rushwa, jambo lililosababisha vurugu kwenye...
  12. M

    Pre GE2025 CHADEMA, kesho 21.01.2025 tuleteeni nuru na siyo giza

    Uchaguzi wa kumpata Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa kesho una maana kubwa sana kwa Taifa letu. Ni siku ambayo Historia ya siasa za upinzani Tanzania inakwenda kuandikwa. CHADEMA wanakwenda kuamua ama kuendeleza siasa za upinzani au kuua kabisa. Ukweli wa Mungu ni kwamba, kulingana na mazingira ya...
  13. Rula ya Mafisadi

    Pre GE2025 Emmanuel Chacha: Mbowe akichaguliwa tena Mwenyekiti nitaachana na CHADEMA milele

    Hali si shwari CHADEMA lolote laweza kutoka ni chama kufa au kupona, tuiombee sana CHADEMA
  14. Cute Wife

    Pre GE2025 CHADEMA walia na rafu kuelekea Uchaguzi wa Mwenyekiti. Team Lissu waliwa vichwa ili kumpa ushindi Mbowe

    Wakuu, Mambo yanakuwa matamu huko, Hilda ameweka bandiko kupitia account ya X kuwa mpaka CHADEMA yanatokea mambo ya hovyo ambayo kila wakati wanayapinga wakifanya CCM. Katika orodha hii inasemekana team Lissu kabakishwa mmoja tu, je tutegemee matokeo tofauti hapo kesho. Kama wao kwa wao...
  15. Li ngunda ngali

    Yericko Nyerere: Kama wewe sio mpiga kura usisogee ukumbi wa kupigia kura Mlimani City

    Hao ndiwo wapiga zumali wa bwana Mbowe kwa sasa. Na ndiwo anaowategemea baada ya Uchaguzi watakuwa wasaidizi wake kwenye Chama. Tafakari.
  16. T

    Pre GE2025 Wanachedema walia na yanayofanyika ndani ya Chadema, wadai hayatofautiani na yaliyofanywa na TAMISEMI kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa

    Mara baada ya Twaha Mwaipaya aliyekuwa mgombea wa nafasi ya mjumbe wa kamati kuu Chadema na aliyekuwa mwenezi wa Bavicha katika uongozi uliopita kuenguliwa katika kinyang'anyiro hiko wanachedema mbalimbali kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii wameeleza hisia zao. Kupata taarifa na matukio...
  17. Bams

    Pre GE2025 Ujumbe mahsusi Kwa Wajumbe wa CHADEMA, msiue matumaini ya Watanzania

    Watanzania wana maumivu mengi na hasira kubwa dhidi ya CCM, chama ambacho kimekuwa kama syndicate ya kuwaumiza watanzania walio wengi na kuzineemesha familia chache kupitia kodi za hao wengi wanaoumizwa. CCM imekuwa na kiburi kisichoelezeka. Wananchi, kupitia tume ya Warioba walisema wanataka...
  18. Tlaatlaah

    Tetesi: Kambi ya Lissu ikiongozwa na Lema na genge lake yajipanga kuvuruga uchaguzi wa CHADEMA ngazi ya taifa baada ya kugundua kushindwa vibaya

    Baada ya mahesabu ya mgombea uenyekiti wao kugoma kabisa, na kwamba kura za wajumbe wa mkutano mkuu haziko upande wao licha ya kufanya press conferences wiki nzima kwa kutambulisha wajumbe, wenyeviti na makatibu wa chadema feki, Hivi sasa wanajipanga kuingia ukumbini kwa lengo la kuhakikisha...
  19. mshale21

    CHADEMA leo umeiga nyendo za CCM za kuengua watia nia ujumbe na nyadhifa mbalimbali ndani yako?

    Rip chadema, ndivyo hivyo tunavyokuaga huku wakuu walliokuua maksudi wakipanga namna ya kujipoza mioyo yao kutokana na majeraha uliowaachia? Chadema leo umeiga nyendo za CCM za kuengua watia nia ujumbe na nyadhifa mbalimbali ndani yako? Chadema leo hii umewaliza watu kwa kuwakumbusha...
  20. J

    Kati ya Press hizi mbili za Wenyeviti wa Chadema kundi lipi ni la kweli?

    ..Press conference ya kwanza hii hapa. https://www.youtube.com/watch?v=lFV-oPTTN28 ..Press conference ya pili hii hapa. https://www.youtube.com/watch?v=Eidcj4OZ5AI CC Erythrocyte , Tindo, brazaj, Fundi Mchundo
Back
Top Bottom