chanjo

Chanjo (kutoka kitenzi "kuchanja"; kwa Kiingereza "vaccine") ni dawa ya kibiolojia ambayo inajenga kingamwili dhidi ya ugonjwa fulani.

Dawa ya chanjo huwa na sehemu za vidubini vinavyosababisha ugonjwa fulani. Dawa hutolewa kutoka katika kidubini kilicho hai au kilichokuwa hai. Sehemu zinazotumiwa kwa dawa haziwezi kusababisha ugonjwa lakini zinatambuliwa na mmfumo wa kinga mwilini.

Mara dawa ya chanjo inaingizwa katika mwili, mfumo wa kinga unaanza kutegeneza fingomwili dhidi ya ugojwa huo.

Chanjo ni njia bora zaidi kuzuia magonjwa ya kuambukiza. Kinga inayoenea kutokana na chanjo kwa kiasi kikubwa inawezesha kuepukana na kifua kikuu duniani na kizuizi cha magonjwa kama vile polio, pepopunda, tetekuwanga kutoka duniani kote. Hata hivi karibuni kumekuwa na mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 kuna chanjo zilitengenezwa na kuukabili

Tunashauriwa na wataalamu wa afya na wanasayansi wa kimataifa kuwapa watoto wadogo chanjo ili iwakinge dhidi ya magonjwa na maradhi mabaya. Kinga ni bora kuliko tiba.
  1. J

    Malaria yapata Chanjo na WHO imeithibisha, utafiti ulianza mwaka 1980

    Uingereza imefanikiwa kutengeneza chanjo ya Malaria ugonjwa unaosumbua sana Afrika. Majaribio ya Chanjo hii yalifanyika katika nchi tatu za Ghana, Kenya na Malawi ambapo watoto zaidi ya 800,000 wamechanjwa. Chanjo hii imelengwa maalumu kwa ajili ya Afrika hivyo nchi zote barani humo zitapatiwa...
  2. Gharama za vifurushi zimepanda kwa asilimia 100

    Hili suala kwakweli limekuwa baya sana. Kadri siku zinavyosonga, maisha ya watu yanazidi kutegemea mtandao. Na kwa kawaida teknolojia inavyozidi kukua ndivyo bei inapozidi kushuka. Sasa inakuwaje hawa jamaa wanaongeza bei kwa asilimia 100. Kwa Tsh 1000 nilikuwa napata GB 1 ya tigo. Sasa napata...
  3. #COVID19 Chanjo zimefika hapa msikitini leo

    Leo mida hii ya swala ya adhuhuri afisa chanjo amefika msikitini tunapo swalia, nahisi atakuwa sio muislam maana kipindi tunaingia kuswali yeye alibaki nje. Baada ya swala watu wachache wamejitokeza kuchanja hasa idadi kubwa ikiwa ni wazee wenye umri zaidi ya miaka 50+ na vijana wachache...
  4. #COVID19 Tuliopata Chanjo ya UVIKO-19 Tukutane hapa. Nini kilikutokea ulivyoipata?

    Salam, Mimi nilipata chanjo ya Jenssen! Good thing sikukutana na changamoto yoyote ile zaidi ya maumivu ya kale kasindano. Na uchovu kidogo kwa saa chache sana. Hii kinga ni nzuri. Vipi ndugu zangu mliopata Chanjo ya UVIKO 19. Wewe ulikutana na changamoto gani? Karibu uhamasishe na wengine...
  5. Kuna Mpango Unaandaliwa Kutumia Vilabu vya Ligi kuu ili Kuchanja Mashabiki Chanjo ya Corona-19

    Kuna mpango mkakati uko juu unaandaliwa. Mpango huo unahusisha kuvitumia vikamilifu vyama vya michezo mbalimbai nchini hasa Mpira wa miguu ili ku-push idadi ya watu ambao hawaja chanjwa ili wachanjwe. Kutatokea na kikao cha siri baadhi ya watu wale walio simamisha mechi ya simba na yanga na...
  6. Achana na Chanjo ya UVIKO-19, Hii ndio propaganda nzito iliyokuwa inapigwa kupinga Umeme miaka ya 1990s

    Propanda ya kupinga Umeme.
  7. L

    #COVID19 Matumizi ya sheria yatasaidia kuhakikisha Watanzania wote wanaostahili kuchanjwa chanjo ya COVID – 19 wanachanjwa kwa wakati, hakuna kubembelezana

    Kwa mujibu wa sheria ya afya jamii ya mwaka 2009 (Public Health Act, 2009) kifungu cha 24, imeeleza kuwa ni lazima kuchanjwa wala sio hiari. Na kila aliyechanjwa anapaswa kuwa na kadi/cheti. Vilevile, kifungu hicho cha 24 (2) kinatoa adhabu ya shilingi laki moja au kifungo cha miezi mitatu au...
  8. #COVID19 Kuagiza chanjo ya Covid-19 kabla ya kutoa elimu kwa raia ni matumizi mabaya(Misallocation)

    Mapokezi ya chanjo ya COVID19 nchin sio mazuri, mikoa mingi wana chanjo nyingi zimebaki na watu hawajitokezi kuchanja. Hali hii inataka nchi kujitafakari namna bora ya kuwashawishi wananchi ili wakubaliane na chanjo au waweke ulazima wa kupata chanjo hiyo kwa kuweka vikwazo mbalimbali kama...
  9. #COVID19 Simiyu: Mwamko wa Chanjo ya Covid-19 ni mdogo sana

    Mganga Mkuu wa Mkoa, Dkt. Boniphace Marwa amesema Mkoa huo haufanyi vizuri katika mapokeo ya Chanjo licha ya Maambukizi kuwepo pamoja na Vifo vya Wagonjwa. Dkt. Marwa amesema sababu zinazopelekea mwamko mdogo wa Wananchi ni pamoja na sababu za kijamii na Elimu ya Chanjo kutowafikia Watu wengi...
  10. #COVID19 Rais Samia: Nimeona Afisa Afya Tunduru akipita nyumba kwa nyumba kuchanja, suala hili lisifanyike kwa mabavu

    Samia amesema anaunga mkono chanjo ya nyumba kwa nyumba inayopendekezwa na mkuu wa mkoa wa mbeya. Swali hizo cost zinazotumika kulazimisha watu wachanjwe zinatoka wapi? Kwanini pesa zisielekezwe kwenye mambo mengine ya msingi. Mama wanaomshauri wanamponza Sana. --- Rais Samia Suluhu...
  11. #COVID19 Rwanda yafanikiwa kutoa chanjo kwa 10% ya watu wake

    Rwanda imesifiwa kufikia lengo la dunia ambapo kila nchi itapaswa kuchanja walau 10% ya watu wake na hivyo imeondolewa katika orodha ya nchi zilizokuwa katika orodha nyekundu ya kuingia Nchi za Ulaya Rwanda ilipokea dozi milioni 3.4 za chanjo na kuanzia mwezi Agosti hadi Septemba 24...
  12. M

    #COVID19 Serikali imeanza kulazimisha watu kuchanja chanjo za COVID-19?

    Inavyoonekana serikali ya Tanzania imeanza kulazimisha wananchi kuchanja chanjo za Covid bila ridhaa zao. Tumeona mkuu wa mkoa wa Mbeya akitoa kauli za kulazimisha watu huko Mbeya kuchanja ikiwemo wafungwa Sasa kuna kauli tena ya serikali ikiagiza wakurugenzi watendji wa Taasisi za serikali...
  13. E

    #COVID19 Msaada: Hospitali zinazotoa Chanjo ya Pfizer au Mordena

    Habari ya majukumu wapendwa. Ninaomba kujua kama kuna hospital inayotoa chanjo ya Pfizer au Mordena kwa Tanzania hapa.
  14. #COVID19 Tanzania kupokea dozi milioni 2 za chanjo aina ya Sinopharm

    Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema Tanzania inatarajia kupokea Dozi Milioni 2 za Sinopharm kutoka Nchini China. Kwenye chanjo hiyo, mtu atapokea dozi mbili tofauti na Johnson & Johnson ambayo inachomwa mara moja Akizungumza kutoka Mkoani Singida, Msigwa ameeleza kuwa idadi ya...
  15. K

    #COVID19 Chanjo ya COvID19 inaweza isiwe na ubora kwa uhifadhi hafifu.

    Ubora wa chanjo unaendana na kufuatilia taratibu za uhifadhi. Kama chanjo imeelekezwa kutumika kwa kipindi flani lazima iwe hivyo, Kama imeelekezwa kutunzwa kwenye joto la ngazi flan lazima iwe hivyo na Kama imeelekezwa kuwekwa kwenye ubaridi pia inabidi iwe hivyo. Kampeni inayoendeshwa Mikoani...
  16. #COVID19 UNGA: Afrika yaeleza ukosefu wa usawa chanjo za Corona

    Viongozi wa Afrika wameelezea ukosefu wa usawa katika usambazaji wa chanjo za Covid-19, wakati walipohutubia kikao cha 76 cha Baraza kuu la Umoja wa Mataifa, mjini New York. Katika hotuba yake ya kwanza kwa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa, Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema ukosefu wa...
  17. M

    #COVID19 Elimu kuhusu chanjo... Part 2 – uviko 19 (muendelezo wa uzi wa elimu kuhusu chanjo)

    Kabla ya kuendelea tafadhali piti andika linalohusu chanjo kwa ujumla Elimu ya jumla kuhusu chanjo (yoyote inayotolewa hapa nchini) UVIKO 19 NI NINI? Kwa Kiswahili tunaita UVIKO 19, yaani “Ugonjwa wa Virusi vya Korona wa mwaka 2019” ikiwa ni tafsiri sisisi ya maneno “Corona Virus Disease 2019”...
  18. B

    #COVID19 Umoja wa Afrika umeshindwa kutengeneza chanjo ya COVID-19?

    Kuna tatizo kubwa Afrika, Yaani hata kwa kuunganisha Nguvu zetu kwa pamoja kuja na chanjo moja imeshindikana, tunabaki kuwapa pongezi kubwa wazungu kwa kutuletea chanjo. maisha ya mwafrika yapo mikononi mwa mzungu. Sasa tuna Uhuru gani? Uhuru wa kupandisha bendera na kushusha basi. Uhuru wa...
  19. #COVID19 Rwanda: Waliopata chanjo wataruhusiwa kukukusanyika kwenye sherehe

    Rwanda imelegeza masharti waliyoweka katika kudhibiti maambukizi ya #COVID19. Baa zitafunguliwa na mikusanyiko itaruhusiwa Watakaoruhusiwa kuwepo kwenye mikusanyiko kama sherehe na maonesho ni watu waliopata chanjo pekee. Hatua hizo zitaanza kutekelezwa Septemba 23 Hatua hiyo imefikiwa baada...
  20. #COVID19 Anne Makinda: Sensa ya watu na makazi haihusiani na chanjo

    Kamisaa wa Sensa, Anne Makinda amesema baadhi ya watu wana imani potofu kuwa zoezi la uhesabu watu na makazi wanahusiana na chanjo ya #COVID19 Amesema hilo sio kweli, japo ni muhimu kwa wananchi kupata chanjo ya corona. Ambapo wanaendelea kutoa elimu kuhusu sensa itakayofanyika 2022 Aidha...
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…