Mgeni siku ya kwanza
mpe mchele na panza;
mtilie kifuani,
mkaribishe mgeni.
Mgeni siku ya pili
mpe ziwa na samli;
mahaba yakizidia,
mzidishie mgeni.
Mgeni siku ya tatu
jumbani hamuna kitu.
mna zibaba zitatu,
pika ule na mgeni.
Mgeni siku ya nne
mpe jembe akalime.
akirudi muagane,
aende kwao...