DAWASA, sielewi utendaji wao. Sisi wakazi wa Ukonga karibu na Aviation House, ni mwezi sasa maji hayatoki. Kuna tatizo la kutoboka kwa bomba kubwa Mlima Ukonga, lakini licha ya DAWASA Kinyerezi kupewa taarifa, hakuna kinachoendelea mpaka sasa kulitengeneza bomba hilo ili tuweze kupata maji.