Huu ni mwaka wa 70 tangu China kutoa Kanuni Tano za Kuishi Pamoja kwa Amani. Miaka 70 iliyopita, aliyekuwa Waziri Mkuu wa China Zhou Enlai alipendekeza kwa mara ya kwanza kanuni tano za “kuheshimiana mamlaka na ukamilifu wa ardhi, kutovamiana, kutoingilia mambo ya ndani, usawa na kunufaishana...