Rais Steinmeier ambaye yuko ziarani nchini Tanzania, amezungumzia kusikitishwa kwake na kile alichokiita fedheha ya uhalifu uliofanywa na Ujerumani wakati ilipokuwa ikiitawala Tanzania, enzi za Ukoloni.
Vita vya Majimaji, vilivyotokea kati ya mwaka 1905 na 1907, ilikuwa harakati za upinzani...