Leo nimechafukwa kupita maelezo!
Hivi nyie Vodacom Tanzania kwanini mnaniibia? Kwanini mnaniunga na huduma bila ridhaa yangu na kuanza kufyeka salio langu? Cha kusikitisha nilipowapigia watoa huduma wenu (customer care) wanasema eti nilijiunga na huduma inaitwa SOKA LETU, jamani Vodacom...