JESHI la Magereza linakusudia kuongeza vifaa vya upekuzi magerezani na kufunga kamera za usalama za CCTV, ili kubaini vitendo viovu vinavyofanyika ndani ya magereza hayo.
Hayo yalisemwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakati ikijibu swali la Mbunge Viti Maalumu, Rukia Kassim Ahmed (CUF)...