Watanzania salamu, ndipo nashika karamu, Naleta jambo muhimu, Fungua zenu fahamu, Umasikini Ni sumu, unaoleta magumu, kujituma ni silaha,na kazi iendelee.
Ukilala ni hasara, utaitwa ni fukara, omba omba inakera, kwa wengi unajichora, fanya kazi barabara, kipato kiwe imara, kujituma ni silaha...