SHAJARA YA MWANAMZIZIMA:
MJUE ‘MAMA KIZIMKAZI’ NA KWAO!—1
Na Alhaji Abdallah Tambaza
ILIKUWA ni Jumapili angavu yenye nuru tokea kulipopambazuka asubuhi, Agosti 21, mwaka huu, mbele ya jumba jeupe (Ikulu) la Makao Makao ya Serikali, kijijini Chamwino, yapata kilometa 35 kutoka Dodoma, mjini...