HALI ILIVYO RWANDA: Dereva wa Lori kutoka #Tanzania haruhusiwi kuvuka Mpaka wa Rusumo ili kuepuka kuingiza Corona nchini humo.
Badala yake; akifika kituo cha Kiyanzi, mzigo wote utapuliziwa dawa kisha atakabidhi Lori kwa dereva wa Rwanda ambaye atalipeleka hadi kituo cha mwisho. Serengeti Post...
Baada ya kunyanyasika vilivyo nchini Rwanda madereva wa malori wa Tanzania wamejichukulia sheria mkononi kuyazuia malori yote kutokea Rwanda kuingia nchini.
Inasemekana baada ya Rwanda kuudhibiti ugonjwa wa Corona vilivyo nchini mwao, kitisho pekee kwa sasa kimebakia kuwa kutokea kwa wageni...
Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza hatua mpya za kudhibiti mienendo ya madereva wa malori yanayoingia nchini humo kutoka mataifa jirani baada ya zaidi ya madereva 20 kupatikana na ugonjwa wa Covid-19.
Mataifa ya Uganda na Kenya yamekuwa yakiwafanyia vipimo wa virusi vya corona madereva...
Serikali imetolea ufafanuzi kuhusu Idara ya Uhamiaji nchini Zambia kuwazuia madereva wa IT katika mpaka wa Tunduma Mkoani Songwe kuingia nchini Zambia, ikiwa ni katika kujikinga na Virusi vya Corona.
Mkuu wa Wilaya ya Momba mkoani Songwe, Juma Said Irando ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya...
Waziri wa Ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Injinia Isack Kamwelwe amesema serikali iko mbioni kuwasajili madereva na makondakta wa daladala ili kuboresha Huduma hiyo hapa nchini.
Mh Kamwelwe amesema kabla ya kusajiliwa watendaji hao wa kwenye daladala watalazimika kupelekwa darasani na kupatiwa...
Uzi huu uwe maalum kwa madereva na wasafiri kujua hali ya barabara ni haki yenu kabla ya kuanza safari ya huko uendako.Tupashane yanayojiri ili tuweze kusaidia safari zetu. Unatarajia kuelekea wapi saa hizi, unahitaji kujua hali ya barabara kama labda kuna changamoto yeyote saa hizi ili kuepusha...
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema inakusudia kutunga Sheria ya Adhabu ‘’papo kwa papo’’ ili kudhibiti ajali, ambazo zimekuwa zikisababisha vifo vya wananchi wengi wa Zanzibar.
Hayo yalisemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mustafa Aboud Jumbe wakati...
Madereva wametakiwa kuwa waangalifu katika kuhakikisha usalama wa abiria hasa katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka kutokana na uzoefu wa huko nyuma kwamba kipindi kama hiki hutokea ajali nyingi.
Ameyasema hayo Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, Kamishna Msaidizi...
Fani ya udereva wa magari imetoa ajira kwa wazee na vijana katika nchi yetu.
Katika kazi hii kuna changamoto mbalimbali wanazopitia ikiwemo kusafiri umbali mrefu.
Kuna mkasa mmoja jamaa alikuwa dereva wa bosi mmoja masharti ya yule bosi lazima dereva awe analala ndani ya gari na pia...
KUGUNDULIKA kwa gesi kwenye mikoa ya Kusini mwa nchi, kumeokoa fedha nyingi ambazo zilikuwa zikitumika kununua petroli na dizeli. Hayo yameelezwa na wafanyabiashara wa kusafirisha abiria jijini Dar es Salaam kwa nyakati tofauti.
Mmoja wa watu hao ni dereva teksi aliyejitambulisha kwa jina moja...
Huu uzi ni kwa ajili ya madereva wa Uber ku-share mikasa wanayokutana nayo katika kazi zao. Nimeamua kuuanzisha baada ya dereva mmoja kunisimulia mastory ya abiria anaokutana nao hasa nyakati za usiku siku za weekend wakiwa wamekolea.
Hivi vituko vinavoendeleaga vinawakuta na wengine? Nina hamu...
Sisi madereva wa magari makubwa hususani malori tunanyanyasika sana barabarani imefikia hatua hata ya kuichukia serikali yetu inayoongozwa na mtukufu Rais Dkt. John Pombe Magufuli tunaimani sana na Rais wetu huyu kwa utendaji kazi wake wenye kuleta maendeleo nchini na mtetezi wa wanyonge lakini...
Madereva wenye uzoefu na kazi na wanaoijua kazi wanapatikana kwa wakazi wa Dar es salaam ,Dodoma na Mwanza.
SIFA ZAO
★Wanajua ufundi wa magari
★Wamepitia mafunzo ya udereva
★Hawana rekodi mbaya ya kutokamilisha hesabu
★wastaarabu
★Wasafi
Wasiliana na sisi tunguunganishe moja kwa moja na dereva...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.