Kiukweli huyu Mama Mkwe ni mwisho wa reli. Ananibamiza haswa.
Kabla ya ujio wake, nyumbani kwangu palikuwa swalama waswalamanta. Lakini tangu aje hapa pamegeuka kibiti, ananinyuka kama kifaranga.
Ana gubu kali, ukikohoa anasema unamcheka, anakubutua na mwiko. Nimevimba kila mahali, uso wangu...