Dar es Salaam–Mwanamuziki nyota wa Bongo Flava, Omary Ally Mwanga, anayefahamika kwa jina la kisanii Marioo, ametambulishwa rasmi kama Balozi wa Bahati Nasibu ya Taifa ya Tanzania. Ushirikiano huu wa kimkakati unaleta matumaini, burudani, na fursa zinazoweza kubadilisha maisha ya Watanzania...