Taarifa ya Jeshi la Polisi imesema Januari 24, 2025, saa kumi na mbili jioni katika Kijiji cha Kilulu Kata ya Bunamala Tarafa ya Ntuzu wilayani Bariadi, Jeshi la Polisi kupitia kikosi kazi cha kupambana na uhalifu, kilifanikiwa kumkamata Emmanuel John Maduhu (31), Msukuma na mganga wa kienyeji...