Wakazi wa Mtaa wa Chinyoya, Kata ya Kilimani, Wilaya ya Dodoma Mjini, jijini Dodoma, wamepinga uteuzi wa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) anayewania nafasi ya uenyekiti, wakidai kuwa mgombea huyo ameonesha tabia za kujifanyia maamuzi kwa matakwa yake binafsi na kutumia ubabe katika uongozi...