Mimi ni mfuasi wa upinzani, sijui Lissu yupo wapi? Nilimsikia na kumuona alipotoka Belgium na kufanya mkutano wa hadhara hapa Dar. Baada ya hapo hajasikika tena.
Nimekuja hapa JF kwa kujua nitapata majibu alipo Lissu, tafadhali naomba kujua.
Nimefuatilia mikutano ya CHADEMA kila kona ya nchi inaonekana mikutano hiyo ni mbinu za ccm kumchafua Magufuli na wananchi wahisahau au wasitambue ufisadi unaoendelea nchini.
Ninaomba michango yenu.
Baada ya rais wa Tanzania kuruhusu mikutano ya hadhara mimi nilijiuliza ni ajenda zipi wapinzani wanapaswa kwenda nazo?
Pongezi Kwa mama Kwa kuruhusu mikutano?
Katiba mpya ambayo pia mama kasema anataka mchakato wake uanze?
Kupanda kwa bei ya chakula ambapo pia unahitaji uangalifu maana...
Mwenyekiti Chadema, Freeman Mbowe anatarajiwa kuzindua rasmi kanda ya Nyasa Februari 23 wilayani Sumbawanga Mkoa wa Rukwa na kisha kufungua mkutano wa hadhara mkoani Iringa Februari 28 mwaka huu.
Hayo yameelezwa Jumanne Februari 21, 2023 na Mwenyekiti wa Chadema wa mkoa huo, William Mungai...
MBOWE NA ZITTO KWANINI WAMEAMUA KUZIACHA HOJA ZA WANANCHI MIKUTANO YA HADHARA
Nimefuatilia mikutano ya hadhara ya Chadema na ACT Wazalendo sijawasikia Mbowe wala Zitto wakizungumzia au wakipaza sauti zao juu ya mambo makubwa yanayolalamikiwa na wananchi.
Mfano suala ulinzi wa rasilimali za...
Kwa mara ya kwnza tunashuhudia upinzani wa aina yake nchini Tanzania, upinzani ambao unaacha kupigana na utawala uliopo na badala yake unapigana na kivuli cha marehemu Magufuli.
Naomba ieleweke kuwa hili halitokei kwa bahati mbaya, Zitto Kabwe kukejeli ndege zilizonunuliwa na Serikali ya...
Wakuu,
Jamaa wameruhusiwa kufanya mikutano ya kisiasa waliyokua wanalilia kila wakati, inashangaza mbona hawana hata hoja za maana?
Haikuepo sababu kabisa kuwazuia wasifanye mikutano, ukiwasikiliza hawana hoja yenye mashiko hata moja. Kwa aina ya wapinzani hao kuchukua dola kwanza wasahau...
Nilikuwa najiuliza kwanini wabunge wameanza kuongea kishabiki kwenye bunge hili? Jibu kumbe ni mikutano ya hadhara. Wemekuwa waki lalama kama vile wenyewe ni wapinzani na kupuuza ukweli wa mambo. Kizuri Bashe amekuwa anajua data kuliko wenyewe. Mikutano kuruhusiwa tu sasa tumeshaanza kuona...
Ndugu zangu watanzania,
Hivyo Ndivyo unavyoweza kusema,kwa wafuatiliaji wa siasa Tuliona mapema kuwa upinzani utapata shida kubwa Sana majukwaani katika kujenga hoja zenye kuwashawishi na kuteka Hisia za Watanzania,kutokana na sababu kuwa Rais Samia amefanyia kazi kero na changamoto mbalimbali...
WanaJamvi nimefuatilia Hotuba za Mikutano yote ya hadhara iliyofanyika baada ya Mama Samia kuifungua.
Kwa maoni yangu mpaka sasa Mnyika anaongoza kwa kutumia nafasi hizo vizuri. Ukimuangalia kwa muda mchache anaopewa anaongea point tupu na kugusa mambo ya Msingi ikiwemo Katiba Mpya, Maisha ya...
Ukweli usiofichika mikutano ya CHADEMA imekosa mvuto. Watu walikuwa wachache sehemu zote walizofanya. Na ikageuka kuwa mikutano ya wanachadema. Haina tofauti na vikao vya ndani vya chama.
CHADEMA inapaswa kujua sababu ya yote hayo ni nini, sikubaliani na wanaosema eti mwenyekiti Mbowe ndio...
Imebidi niulize ili labda kama kuna anayejua ratiba ya Mikutano ya hadhara ya Wanasiasa hawa na vyama vyao atueleze.
Mchumi Lipumba na Bwana Mapesa ni wanasiasa wakongwe mno, bila shaka wataitumia fursa hii ya mikutano ya hadhara ili kuimarisha vyama vyao.
Siku moja baada ya CHADEMA kuzindua mikutano ya hadhara jijini Mwanza, Chama cha ACT Wazalendo nacho kimetangaza kuanza mikutano yake Februari 19, 2023 jijini Dar es Salaam.
Akisoma maamizio ya kamati kuu ya chama hicho iliyoketi jana Dar es Salaam, katibu mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu...
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema uamuzi wa kuzuia mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa haukuwa wa Hayati John Magufuli pekee, bali na uongozi wa chama chake- Chama cha Mapinduzi (CCM).
Mbowe ameyasema hayo leo Jumapili, Januari 22, 2023 katika mkutano wa hadhara uliofanyika...
Nahisi Mwenyekiti Mbowe amelewa, hii sio sauti yake ya kawaida. Ametumia mkutano huu kujisafisha kuhusu kulamba asali.
Japo Rais Samia Suluhu anafanya vziuri lakini ametumia muda mrefu sana kumsifia.
Is MBOWE OKAY?
Hawa vijana wa CHADEMA waliojazana humu na kutoa maneno ya kejeli kumbe ni bure kabisa.
Ni bure kiasi kwamba hawawezi kuongea kwenye mikutano ya hadhara na ndiyo maana wameahirisha kuanza mikutano ya hadhara hadi Lissu, Lema, na Wenje waje.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amewasihi waandishi wa habari kuepuka kuandika maneno yasiyo ya staha na kuegemea upande mmoja wakati wa mikutano ya vyama siasa iliyoruhusiwa na Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni.
Nape alienda mbali zaidi na kusema...
Taarifa zilizotoka za kuruhusu mikutano ya hadhara ya kisiasa hapo majuzi zinadai kuwa mikutano hiyo ilizuiwa baada ya baadhi ya wanasiasa kufanya mikutano hiyo kuwa pango la matusi,kashfa na uchochezi.
Hebu kwa uchache tukaone haadhi ya video za wanasiasa hao
1. Je wamponde Samia wamsifie magufuli ?
AU
2. Wamsifie Samia wamponde Magufuli?
AU
3. Wamponde Awamu zote za CCM?
Naona wanawakati mgumu kupata hoja maana wananchi tunamini Katika Magufuli hatuna imani na samia
Ila wapinzani hawaamini Katika magufuli Wana imani na samia. Nasubiri Kwa hamu...
Katika ulimwengu huu wa kidigitali kila kitu kinaweza kufanyika kwa urahisi, uhakika, na ufanisi mkubwa kwa kutumia teknolojia ambazo hazihitaji watu kukusanyika na kukutana mwili kwa mwili. Lakini hapa Tanzania naona kama ni tofauti. Hili limuejidhihirisha kwa jinsi watu walivyokamia mikutano...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.