Takwimu zilizotolewa karibuni na Shirika la Afya Duniani (WHO) zimeonesha kuwa, kuanzia tarehe 13 mwezi Mei, nchi 12 zimeripoti kesi 92 zilizothibitishwa za maambukizi ya virusi vya monkeypox, na kesi nyingine 28 zinazoshukiwa, na mpaka sasa hakuna vifo vilivyoripotiwa kutokana na ugonjwa huo.