Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linawashikilia mume na mke, wakazi wa mtaa wa Mji Mwema manispaa ya Songea kwa tuhuma za kuiba mtoto mwenye umri wa miezi 11 (jina limehifadhiwa).
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Marco Chillya amesema tukio hilo limetokea Novemba 4, 2024...