THAMANI YA MTU MWEMA, HUNG’ARA AKISHALALA!
Tenda wema nenda zako, msemo tangia enzi,
Timiza wajibu wako, kwa watu na kwa Mwenyezi,
Iache alama yako, kwa kizazi na vizazi,
Thamani ya mtu mwema, hung’ara akishalala!
Wema msalaba wako, ubebe bila simanzi,
Wema ni hazina yako, isiyoibwa na wezi...