Dar/mikoani. Ni machozi ya damu, ndivyo unavyoweza kueleza katika simulizi ya vifo vya mfanyabiashara wa madini, Mussa Hamis anayedaiwa kuuawa na maofisa wa polisi, huku ofisa wa jeshi hilo, Grayson Mahembe aliyekuwa akishikiliwa kwa tuhuma hizo akidaiwa kujinyonga hadi kufa akiwa mahabusu...