SERIKALI imesema Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), itaanza kupandikiza chembechembe hai kwa wagonjwa wa saratani ya damu kuanzia Machi mwaka huu.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima, alitangaza neema hiyo jana alipozuru katika hospitali hiyo...