Wanachama wa chama cha mapinduzi, wilaya ya Hai, huko Kilimanjaro, wameshinda ofisi ya chama Wilaya, wakimtafuta Mwenyekiti wao wa Chama Wilaya, siku ya 5 Sasa haonekani.
Mwenye taarifa za kupoteza kwake tafadhali!
Ni kitu gani ambacho bado Mbowe hajakamilisha kinacho muweka kwenye kiti cha uenyekiti hadi sasa? Naomba nitajiwe.
Upi mbadala wa Mbowe katika kiti cha uenyekiti wa chama?
Uenyekiti wa Mbowe wa kipindi kirefu una faidi zipi na hasara zipi katika demokrasia na ukuaji wake?
KENYA: Rais William Ruto amependekeza Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) kumuunga mkono Waziri Mkuu wa zamani na Kiongozi wa Upinzani, Raila Odinga anayewania nafasi ya Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC).
Akihutubia kikao cha EALA, Rais Ruto amesema Viongozi Wakuu wa...
Mwenyekiti wa Chama cha ACT – Wazalendo, Juma Duni Haji maarufu kama Babu Duni amejiondoa kwenye kinyang’anyiro cha uenyekiti ACT – Wazalendo na kumuunga mkono makamu wake, Othman Masoud Othman.
Babu Duni amejiondoa kutetea nafasi hiyo aliyokuwa akihudumu kabla ya muda wake kuisha leo Jumatatu...
Abdul Nondo ametangazwa kuwa mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ya ACT Wazalendo Taifa kufuatia uchaguzi mkuu wa ngome hiyo uliofanyika jana, Alhamisi Februari 29, 2024 kwenye ukumbi wa Hakainde Hichilema uliopo makao makuu ya ACT Wazalendo (Maalim Seif House) Magomeni, Dar es...
Ni ushauri tu kwa ndugu yetu Ndugu Hamis Nyamsenda,Mwenyekiti wa mtaa wa Nyerere ulio katika halmashauri ya mji wa Bunda.Binafsi andiko hili halina maana kwamba tunakuchukia bali tumeamua kufanya haya ili ubadilike na kuwa kiongozi bora.
Binafsi umekuwa ukiitisha mikutano ya hadhara ambapo...
Umoja wa Maafisa Watendaji Wakuu Tanzania wakiwemo wa Mashirika Binafsi na Serikali (CEOrt) wakishirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira (Journalists' Environmental Association of Tanzania – JET) wamekutana na Wadau mbalimbali katika warsha ya kujadili mambo mbalimbali kuhusu...
Mwenyekiti wa Vijana CCM (UVCCM), Kata ya Bwilingu (Chalinze-round about) Ndugu Abdul Nasa ameendelea kukitumia vibaya cheo cha baba yake (Diwani Kata ya Bwilingu Jimbo la Chalinze).
Inadaiwa alifanya jaribio la kujeruhi na kushindwa kuchukuliwa hatua yoyote ya kinidhamu ndani ya chama kutokana...
Hassan Wakasuvi enzi za uhai wake
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimepokea kwa masikitiko na huzuni kubwa taarifa ya kifo cha Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora na Mjumbe wa Kamati Kuu Ndugu Hassan Wakasuvi kilichotokea Leo tarehe 22 Februari, 2024 Mkoani Tabora.
Chama Cha Mapinduzi kitamkumbuka...
Huwa siwaelewi watu wanaowapinga team kataa ndoa na Atheist sababu kufanya hivyo ni kama kupangiana jinsi ya kuishi hapa duniani na hiyo sio sawa kwani kila mtu ana haki ya kuishi na kuamini anachoamini ilimradi havunji sheria wala kubughudhi wengine.
Kataa ndoa sio kitu kipya na ukweli hawa...
Mnamo Februari 9, 2024 katika Mahakama ya Wilaya ya Uyui, mbele ya Mh. Tausi Mongi, imefunguliwa kesi ya jinai (Criminal case No. 20240209000003354) Jamhuri dhidi ya GEORGE FICHA MANYAMA (Mwenyekiti wa Chama cha Wauza Mikaa - UWAMUKU - Tabora). Kesi imefunguliwa na waendesha Mashitaka wa...
Hili hapa andiko la Mhandisi Ndolezi Petro ambaye ametangaza nia ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti Ngome ya Vijana ACT Wazalendo Taifa katika uchaguzi utakaofanyika tarehe 29 Februari, 2024:
UONGOZI NI VIJITI VYA KUPOKEZANA NAMI NAJIANDAA KWENDA KUCHUKUA KIJITI
Mhandisi Ndolezi Petro, Waziri...
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Morogoro, imemkamata na kumfikisha mahakamani Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa shule, Suleiman Mwishehe kwa tuhuma za kujaribu kumhonga Afisa wa TAKUKURU kwa kutoa shilingi Milioni 3 ili asifikishwe mahakamani wakati wa uchunguzi kwa...
KOMREDI RAJABU ABDURRAHMAN ACHANGIA MILIONI 10 UJENZI WA ZAHANATI KIJIJI CHA MWEMBENI
"Katika kuitekeleza ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 nimechangia Tsh 10,000,000/ (milioni kumi) kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati katika Kijiji cha Mwembeni, Kata ya Madanga wilayani Pangani" - Komredi Rajabu...
Diwani wa Kata ya Ilenda, Halmashauri ya Buchosa, Sengerema mkoani Mwanza kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mneke Mauna anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, akituhumiwa kumshambulia na kumpiga makofi Mwenyekiti wa CCM wa kata hiyo, Lazaro Lubalika.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa...
Salaam ndugu zangu,
Nimekaa mtaani kwetu hapa takribani Miaka mitatu lakini sikuwahi kumjua Wala kumuona Mwenyekiti Wala Diwani wa Mtaani kwetu.
Tumekuwa tukipata shida za Maji, changamoto za kijamii lakini daima sikuwahi kumuona. Lakini Mwaka huu tangu uingie nimemuona zaidi ya mara tano...
Miezi kadhaa iliyopita Rais wa JMT alimteua George Nathanael Mandepo kuwa Katibu mtendaji wa tume ya kurekebisha sheria. Leo tarehe 25 January baba Askofu wa Kanisa Anglikana Tanzania dayosisi ya Dar es salaam Rev Jackson Sosthenes Jackson amemuweka Wakfu Adv Mandepo kuwa Shemasi (mchungaji)...
Chama cha ACT Wazalendo kinafuatilia kwa karibu mwenendo wa mambo katika mjadala wa kitaifa unaoendelea kuhusu Miswada ya Sheria ya Tume ya Uchaguzi, Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani.
Ikumbukwe kuwa msimamo wa ACT Wazalendo ambao unatokana na azimio...
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kisokwe wilayani Mpwapwa, Mkoa wa Dodoma, Patrick Nyangauya amekutwa amefariki dunia na mwili wake kutupwa kwenye mtaro na kufunikwa na majani.
Akizungumza leo Jumatano Januari 17, 2024 kijijini hapo, Mtendaji wa Kijiji cha Kisokwe, Anna Fundichuma amesema alipigiwa...
Habari Wana JF.
Kwanza nielezee masikitiko yangu kwa kauli ya Jana ya Mwenyekiti wa CHADEMA Mheshimiwa Mbowe kwamba anajuta kumwamini Rais Samia
Mheshimiwa Mbowe alipigiwa kelele sana kuhusu kuingia maridhiano na CCM hakusikia kabisa. Nakumbuka kwenye mkutano wa CHADEMA Mwanza, tarehe...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.