Kesho Tanzania itapokea ndege ya mizigo. Hatua hii ichukuliwe kwa uzito wa pekee na wafanyabiashara wakubwa na wadogo. Ndege hiyo kubwa ya mizigo aina ya Boeing 767-300F itakuwa na uwezo wa kubeba tani 54 za mizigo na kusafiri katika nchi za Ulaya, Asia na kwingineko ambako soko litapatikana...