Ndoa za utotoni ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu kwa wasichana. Sheria ya Elimu nchini Tanzania, ya mwaka 1978 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2016 inapiga marufuku ndoa za wanafunzi; hata hivyo, Sheria haijasema lolote kuhusu wasichana ambao hawako shuleni na kwa umri wao wangepaswa...